NA HERI SHAABAN


CHAMA cha Walimu (CWT) Wilaya ya Ilala kimeikumbusha Serikali ilipe malimbikizo ya mishahara ya madeni ya walimu.


Hayo yalisemwa katika mafunzo ya viongozi wa chama cha Walimu CWT Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam jana na 

Katibu wa CWT Halmashauri ya Dar es Salaam Erasmo Mwingira wakati wa kusoma risala  yao


Katibu wa CWT Halmashauri hiyo Mwingira alisema 

Serikali wanaidai pesa nyingi sehemu ya malimbikizo ya mishahara yao na madeni ya fedha za likizo pia hawajalipwa.


" Kazi yetu ya Walimu ni wito lakini ina changamoto mbalimbali  tunakabiliana na Changamoto kubwa katika madai ya fedha zetu muda mrefu madai yetu ya fedha za likizo na mishahara atujalipwa ndio tunatumia fursa hii kutoa kilio chetu Kwa Serikali itukumbuke " alisema Mwingira.


Mwingira alisema changamoto nyingine fedha za likizo Kwa Walimu wastaafu kutorudishwa mwakao pamoja na Walimu waliopo Kazini


Alisema wanatimiza majukumu yao ipasavyo lakini madai wanayodai ni makubwa  madeni ya likizo ya uhamisho na masomo jumla shilingi 2,504,058,165

Kati ya fedha hizo Elimu ya msingi wanadai shilingi 1,522,218,881,na Elimu sekondari 981,839,284


Aidha alisema malimbikizo yao  yana  sua sua ya mishahara yao hawalipwi Kwa wakati  hivyo kupelekea changamoto mbalimbali katika kada ya Walimu.


Akizungumzia Walimu waliostaafu kwa daraja la TGTS F lakini waliokokotolewa mafao kwa TGTS E yaani daraja la chini hali  inapelekea wastaafu kufatilia mafao bila mafanikio .


"Serikali yetu ni sikivu  tunaomba Serikali ipeleke michango ya Walimu PSSSF  ili Walimu wastaafu wakokotolewe upya mafao.


  

Aliomba chombo chao TSC kiboreshwe na kujengewe uwezo ya kuwalipa  wa kuwalipa mishahara Walimu na kusimamia shule binasfsi .


Pia alisema mwaka 2015/2016 baadhi ya Walimu walipanda daraja baadae Serikali ilitoa mwongozo ya kutoboresha ili kupisha zoezi la uhakiki kwa watumishi wote wa umma lakini baada ya zoezi la uhakiki   kukamilika  Walimu walipanda daraja 2015/2016 walinyanganywa madaraja yao na kupewa barua mpya November 2017 na wengine April 2018 na kufuta barua zao ilipofika 2021 Walimu waliostahili kupanda daraja barua zao zilifutwa na kupandishwa upya.


  Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu CWT Temeke Nuruel Kavishe aliwataka Walimu wawe wawazi wanapopokea pesa za Serikali za miradi wawe wanatolea Taarifa na kazi wanayozifanyia.


Mwenyekiti wa CWT   Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam Emanuel Kihato alisema  vyama vyote vya Walimu lazima viwashirikishe Walimu  katika kuwasikiliza na kujadili changamoto zao.


Mwenyekiti wa CWT Emanuel alisema Serikali yetu ni sikivu  Ione namna ya kuwapandisha madaraja Walimu hao ili waweze kwenda sawa na wezao 


Emanuel alisema mafunzo hayo yamewashirikisha  Sekondari na idara ya Elimu msingi ,Sekondari Maafisa Elimu kata ,vituo vya Walimu na wadhibiti ubora wa Elimu 


Emanuel alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapandisha madaraja Walimu 2121 kati yao Walimu wa shule za Msingi 1131 na Sekondari 990 na kurekebisha mishahara yao kwa wakati  ndani ya miezi miwili kwa Walimu wote.


Mgeni rasmi Mwakirishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Frank Sanga alisema changamoto mbalimbali ambazo wanakaliana nazo Walimu atazichukua na kumfikishia Mkuu wa Wilaya Ilala.



Mwisho

Share To:

Post A Comment: