Nteghenjwa Hosseah, Arusha


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,  Dkt. Grace Magembe amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Arusha kwa kutoa chanjo kwa wananchi kwa asilimia 94 ya chanjo ya Janssen iliyosambazwa awali. 


Dkt. Grace ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi na wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Afya  na wadau wa afya mkoani Arusha kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma za afya sambamba na mwenendo wa utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19.


Akizunguma katika ziara hiyo amesema Arusha ni miongoni mwa mikoa iliyofanya vizuri katika utoaji wa chanjo ukizingatia jiographia ngumu  na jamii ya watu wanaopatikana humo.


" Arusha kuna maeneo magumu kufikika kama kata za mbali huko Ngorongoro na Loliondo na jamii ya watu wa huko ni wale wanaoamini sana kwenye mila na desturi lakini hicho hakikuwa kikwazo katika utaratibu  wa utoaji chanjo na wamefanikiwa kutoa chanjo kwa watu 47,750 ukilinganisha la chanjo elf 50,000 walizopokea.


Pia Dkt. Grace amewataka kuendeleza usimamizi huo katika Chanjo ya Sinopharm iliyoanza kutolewa hivi karibuni ambayo inahitaji mtu kuchoma mara mbili ili kukamilisha dozi yake na kwa Mkoa wa Arusha wamepokeza dozi 39,809.


Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela:" uongozi wa mkoa umejipanga kutumia mbinu mbalimbali katika kuhamasisha na kutoa chanjo ya UVIKO-19 kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha."

Share To:

Post A Comment: