NA HERI SHAABAN


MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salam  Omary Kumbilamoto amewataka wazazi wa Wilaya ya Ilala kuwekeza  sekta ya elimu kwa watoto wao 

Wazingatie elimu.


Meya Kumbilamoto aliyasema hayo katika mahafali ya kwanza darasa la saba ya Mtakatifu  St ,JB 'Cottolengo  iliyopo Kata ya Vingunguti wilayani Ilala.


"Nawaomba wazazi wangu wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam tuzingatie elimu kwa kuwekeza sekta ya elimu kwa watoto wetu ili wasome kwa bidii kukuza taaluma" aĺisema Kumbilamoto


Meya Kumbilamoto alisema elimu ni ufunguo wa Maisha Taifa lolote ili liwe na maendeleo watu wake wameendelea kielimu  .


Alisema wazazi wakiwekeza sekta ya elimu Taifa letu litapata wanasayansi,,Madaktari na watalaam  mbalimbali kwa ajili ya kujenga nchi yetu .


Aidha Meya aliwataka wazazi kujenga tabia ya kukagua daftari za watoto wao pindi wanaporudi shule .


Aidha pia aliwataka wazazi wa wilaya ya Ilala kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo .


Katika hatua nyingine Meya Kumbilamoto amekabidhi baskeli ya miguu miwili Wheel Chair kwa mtoto mlemavu ambaye alikuwa awezi kutembea anasoma shule ya S't,JB Cottolengo Vingunguti.


Wakati huohuo Meya alitoa ahadi ya kusaidia vitabu vya shule vyenye thamani ya shilingi 600,000/=

Kwa ajili ya shule hiyo ambayo inamilikiwa na Kanisa Katoliki Tanzania.


Meya Kumbilamoto aliagiza uongozi wa Shule ya Mtakatifu st,JB COTTOLENGO  kuanza mikakati ya kuanda  kidato cha kwanza mwakani Wanafunzi wasome hapo wazazi wasipeleke watoto mbali .Meya alisema atafanya mchakato wa kuwatafutia eneo kwa ajili ya upanuzi wa Shule hiyo.

Share To:

Post A Comment: