Mbunge wa Jimbo la Arumeru magharibi Mhe.John Danielson Palangyo amekabidhi hundi ya milioni 93 kwa vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu vipatavyo 33 kama sehemu ya mkopo wa aslimia 10 utolewao na halmashauri ya Meru kupitia mapato yake ya ndani.


Akikabidhi hundi hiyo Mhe.Palangyo amevitaka vikundi hivyo kutumia fedha za wanazokopesbwa katika lengo walilokusudia ikiwa ni pamoja na kuzirejesha fedha hizo kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine kuweza kipata nao fursa ya kukopa. 


Ameongeza kuwa katika kuinadi sera ya chama cha mapinduzi kulitolewa ahadi nyingi ikiwemo mikopo hiyo ambapo mikopo ya wanawake,vijana na wenye ulemavu ni agenda moja wapo sambamba na uwepo wa dawati maalumu la kuunganisha vikundi na kuvipatia mafunzo ya kusimama fedha za mikopo.


"Mwaka jana nilitembea na ilani ya uchaguzi,niliinadi vizuri na agenda ya mikopo ilikuwepo lakini pia baada ya kunichagua pale ofisini nikaanzisha dawati la kina mama na vijana la kuunganisha vikundi na kuvipatia mafunzo ili watakaokuja kukopa fedha wakaxitumie vizuri waendelee mbele."Alisisitiza


Aidha amesema  kuwa mikopo iliyotolewa katika kipindi cha mwaka 2021 kiasi cha shilingi Milioni 395 mikopo ya wanawake,vijana na walemavu siyo haba kwa halmashauri ya Meru kutokana na jitihada kubwa iliyoelekezwa kwenye vikundi hivyo.


Ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka huu jimbo liliweza kupata fedha za kutengeneza barabara kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 ambapo amewaomba wakala wa barabara TARURA kutowagombanisha viongozi na wananchi wao,wafanyekazi kwa uadilifu ambapo pia amewahakikishia wananchi kuwa ipo ahadi ya barabara za kiwanho cha lami katika jimbo hilo.


Pamoja na hayo Mhe.Palangyo amewataka wananchi wote wa jimbo lake kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ambalo litafanyika mwakani ili kuiwezesha serikali kuu kupata idadi kamili ya watu na makazi.


"Wakati wa kugawa rasilimali za taifa ile sensa ndiyo itatumika katika kuzigawa na kuhakikisha kwamba mgawanyo huo unakuwa niwa haki kwasababu kwenye watu wangi lazima miradi iende kwa wingi ili iweze kukidhi mahitaji ya maendeleo ya wananchi wetu."alisema mbunge huyo


Mhandisi Richard Ruyango Mkuu wa Wilaya ya Arumeru katika makabidhiano hayo ameipongeza halmashauri ya Meru kwa kuendelea kutekeleza sera kwa kutenga asilimia 10 kutoka kwenye mapato ya ndani ya halmashauri na kuhakikisha fedha hizo zinasimamiwa ili ziweze kuwafikia walengwa waliokidhi vigezo.


"Niwapongeze sana halmashauri,watendani,lakinu niwapongeze sana na nyingi ambao unapewa mikopo hiyo kwa maslahi mapana ya vikundi vyetu kwa kukidhi vigezo na vigezo hivyo ndiyo mnaendelea kupata mafunzo kuputia kwa watendaji wenh."Alisema Mhandisi Ruyango


"Huu ni mkakati wa serikali lakini ni mkakatika kupitia kwenye ilani ya chama kwamba fedha nyingi tunazozikushanya kutoka kwenye vikundi hivyo lazima asilimia 10 irudi kwao kwa ajili yakutengeneza maendeleo ya vikindi kwa utaratibu uliokubalika na nchi yetu."alisema Mhandisi Ruyango


Vilevile Mhandisi Ruyango amevitaka vikundi hivyo kutumia fedha hizo walizozipata kwa yale waliyokusudia ili mwisjo wa siku yale mazuri yanayofanywa kupitia CCM yaweze kuonekana pamoja na wao wenyewe kunufaika kwasababu serikali iliondoa riba katika mikopo hiyo.


Awali akizungumza na wanavikundi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Mwl.Zainab Makwinya amesema ana inaimani na vikundi hivyo ambapo atahakikisha asilimia 10 inayotengwa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani wanaipata kwa wakati.


Mwl.Makwinya ameomba ushirikiano wa karibu na viongozi wa Halmashauri hiyo pamoja na chama cha mapinduzi uwepo ili kazi ziweze kufanyika kama zilivyokusudiwa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Jeremia Kishili amesema madiwani wamekuwa mstati wa mbele kupambana ili kuhakikisha vikundi vilivyomo katika kata zao vinapatiwa mkopo kwa maendeleo ya ukuaji wa uchumi wao na taifa kwa ujumla.


"Na niwasifu kina mama kurejesha mikopo wanairusha kwa uaminifu kwani vipo vikundi vichache ambavyo kwa kweli vinasumbua kidogo lakini tunaendelea kuwapa elimu ili warudishe kwa muda kusudi na wenzao waweze kukopa,kwahi niwaombe sana tushirikiane kwa pamoja ili kuweza kuleta maendeleo."alisisita Kishiri


Kishili amewashukuru maafisa mikopo ngazi ya kata kuwajali wananchini na kuwahudumia katika moyo wa upendo ili kuweza kuepukana na malalamiko dhidi yao ya kutofika kwenye maeneo kwa ajili ya utoaji wa elimu ya mikopo kwa wananchi.Aliongeza 


Sambamba na hayo Katibu mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Joshua Mbwana akiwakilisha chama hicho amewataka wananchi kuendelea kuiamini serikali iliyopo madarakani pamoja na viongozi wite wa halmashauri na kuwapa ushirikiano.


Wakati huo huo Afisa mikopo Wilaya ya Meru Bi. Angelina Christian amesema kuwa Idara ya maendeleo ya jamii kwa kusjirikiana na maafisa maendelwo ya jamii kata wameweka utaratibu wa kutembelea vikundi kabla havijapatiwa mikopo kwa ajili ya kuangalia miradi waliyo nayo.


Sambamba na hayo ametoa woyo kwa vijana kutambuwa wanamchango mkubwa katika taifa hivyo amewataka kuchangamkia fursa zinazotokea katika kujishughulisha na shughuli mbalimbali zitakazo waingizia kipato ikiwemo kujitokeza katika uchukuwaji wa fedha za halmashauri.

Share To:

Post A Comment: