Monday, 18 October 2021

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MWENDEHSA MASHTAKA

  


Ferdinand Shayo,Manyara


Mahakama Ya Hakimu Mkazi  Manyara Imemwachia Huru Aliyekua Mwendesha Mashtaka Wa Mkoa Wa Manyara Mutalemwa Kishenyi Aliyekua Akikabiliwa Na Tuhuma Za Kuomba Na Kupokea Rushwa Ya Shulingi Milioni Tano Baada Ya Upande Wa Mashtaka Kushindwa Kuthibitisha Mahakamani .

Akitoa Hukumu Hiyo Hakimu Elimo Daniel Massawe Amesema Kuwa Mahakama Imepitia Ushahidi Wa Pande Zote Mbili Na Kujirisha Kuwa Mwendesha Mashtaka Huyo Hana Hatia Kama Ilivyodaiwa Awali Kuwa Alipokea Rushwa Kutoka Kwa Mfanyabiashara Gasper Mlay Kwa Lengo La Kumsaidia Mfanyabiashara Huyo Ambaye Aliwahi Kuwa Moja Kati Ya  Wakurugenzi Wa Kampuni Inayozalisha Vinywaji Vikali Mkoani Hapa.


Hakimu Massawe Amesema Kuwa Hakuna Shahidi Yoyote Aliyethibitishia Mahakama Hiyo Iwapo Kulikua Na  Mawasiliano Kati Ya Mshatikwa Na Mkuu Wa Upepelezi Jeshi La Polisi Mkoa Wa Manyara  Kwa Lenga La Kumsaidia Gasper Mlay.


Aidha  Hakimu Amesema Kuwa  Takukuru Walipochukua Vieleelezo Kama Pesa Na Simu Havikusainiwa Na Mashahidi Katika Eneo La Tukio Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa Na Badala Yake Vilisainiwa Katika Ofisi Za Takukuru Mkoa Hivyo Vieleelezo Hivyo Havifai Kutumika Mahakamani.


Pia Mahakama Imethibitisha Kuwa Shahidi Wa Upande Wa Mashtaka Gasper Mlay Hakua  Mfanyakazi Wa Kampuni Ya Mati Super Brands Hivyo Hakutumwa Na Mkurugenzi Wa Kampuni Hiyo David Mulokoz Kupeleka Rushwa Ya Milioni Tano Kwa Aliyekua Mwendesha Mashtaka Wa Serikali Mutalemwa.


Hakimu Amesema Kuwa Mahakama Imeona Kuwa Kuna Mashaka Mazito Na Mengi Kwa Upande Wa Mashtaka Kushindwa Kuthitisha Kuwa Mutalemwa Ana Makosa Hivyo Mahakama Imeamua Kumwachia Huru.


Wakili Wa Upande Wa Utetezi Wakili Msomi Thadey Lister Amesema Kuwa Mahakama Imetenda Haki Na Kumwachia Mteja Wake Huru.


Kwa Upande Wake Mwendesha Mashataka Wa Takukuru Mkoa Wa Manyara Martin Makani Amesema Kuwa Wamekubaliana Na Hukumu Iliyotolewa Na Mahakama Hiyo…Insert 2…Martin Makani…Mwendesha Mashataka Wa Takukuru Mkoa Wa Manyara .

No comments:

Post a Comment