Jane Edward, Arusha


Chuo cha uhasibu Arusha(IAA) kimewataka vijana wa kitanzania kuchangamkia fursa ya kozi mpya ya Bima iliyoanzishwa kwa lengo la kuwawezesha vijana hapa nchini kupata ajira kwa urahisi.


Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa tehama uliyomalizika jijini Arusha


Mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha Profesa Eliaman Sedoyeka amesema chuo cha uhasibu kimejipanga kuhakikisha vijana wanaondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kutoa kozi hiyo.


Amesema kuwa kozi ya bima inalenga kumuandaa kijana kuwa mtaalamu wa kujikinga na majanga mbalimbali 


"Kati ya sekta ambazo ajira yake ni rahisi na haitumii mtaji mkubwa ni hii kwakuwa kijana anatakiwa kutafuta wateja kwa kuwafata ili waweze kukata bima ya vitu vyao ikiwemo magari, nyumba, simu, nk" alisema Profesa Sedoyeka



Ameongeza kuwa hii ni kozi ambayo kijana anaweza kusoma akiwa kazini na chuo cha uhasibu ni chuo cha pili hapa nchini kutoa kozi hiyo muhimu.


Amewataka vijana wa kitanzania kutumia fursa hiyo muhimu katika kujikomboa na ukosefu wa ajira na chuo cha uhasibu kiko tayari kutoa elimu hiyo kwa mustakabali wa Taifa.


Share To:

Post A Comment: