Na Mwandishi wetu ,Mbarali


DIWANI wa kata ya Kongolo Mswiswi wilayani Mbarali Mkoani Mbeya ,Elia Bange amekabidhi  vifaa vya shule aina ya printer  na computer kwa ajili ya kuboresha elimu katika kata hiyo .


Diwani Bange amesema kuwa kadri anavyopata fedha  ataendelea kusaidia mahitaji  mbali mbali katika kata hiyo ambayo ina uhitaji wa vifaa hivyo ili kuwapunguzia adha ya kutembea  walimu kutafuta huduma hiyo na badala  yake muda huo utumike kufundisha watoto darasani.


“Leo hii nimekabidhi printer na computer  katika shule ya msingi Azimio Mswiswi  nawashukuru sana wadau wangu  akiwemo Naibu waziri wa maji Mhandisi ,Maryprisca Mahundi (Mb)kwa  kuniunga mkono na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi “amesema Diwani Bange.


 Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Azimio ,Omary Mwambela alipongeza jambo kubwa lilofanywa na Diwani huyo  na kuwataka waau wengine  kusaidia shughuli za maendeleo katika kata hiyo .


“Kwenye hii kata tuna vitu vingi vya kusaidia tunaomba diwani wetu aungwe mkono kwa jitihada hizi anazofanya za kuboresha sekta ya elimu  katika kata hii ,hii inasaidia walimu badala ya kuhaingika  sasa mua huo watatumia kukaa kufundisha watoto wetu”amesema mwananchi huyo.

Share To:

Post A Comment: