Na Mwandishi wetu ,Mbeya


Taasisi isiyo ya kiserikali Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)imetoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni sita kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Machifu liliopo Nane Nane Jijini Mbeya.


Akikabidhi vifaa hivyo  Mtendaji mkuu Miriam William kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amesema Mahundi anatekeleza ahadi yake baada ya kutembelea jengo hilo na machifu kuomba msaada wa vifaa vya ujenzi.


Akipokea vifaa hivyo Chifu Roketi Mwanshinga ameishukuru Taasisi hiyo kupitia Mkurugenzi wake Mhandisi Maryprisca Mahundi kwani msaada wake ni mkubwa.


Aidha Chifu Michael Yilanga na Chifu George Lyoto wameshukuru kupokea vifaa hivyo na kuomba wadau wengine kusaidia ujenzi wa jengo la Machifu.






Share To:

Post A Comment: