Thursday, 2 September 2021

RC MAKALA AMEZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUENDELEZA MAENEO YAO

 NA HERI SHAABAN


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amezitaka taasisi za Serikali na Taasisi za umma kuendeleza maeneo yao ya ardhi.


Mkuu wa Mkoa Amos  Makala aliyasema hayo Wilaya ya Temeke katika ziara yake ya kutatua kero za wananchi .Makala alisema maeneo mengi ya ardhi ya mashirika na taasisi za Serikali yameachwa bila kuendelezwa na kuleta migogoro ya ardhi kufuatia maeneo  hayo kuachwa kiholela.


"Ninaagiza katika mkoa wangu mashirika yote ambayo yanamiliki maeneo Dar es Salaam naomba maeneo hayo yaendelezwe yakiwemo kuyajengea ili kuepusha migogoro ya ardhi kuepuka wananchi kuvamia ardhi kiholela .


Aidha alisema ardhi aitoshi na wavamizi wapo ni muhimu kuyalinda maeneo hayo kwa kuyajenga kwa wakati.


Aliwataka Watendaji wa Mkoa Dar es Salaam kila Wilaya kushughulikia Migogoro ya ardhi  katika Wilaya zao kwa wakati .


Alisema katika ziara zake Leo Wilaya ya NNE kesi kubwa anazokutana nazo migogoro ya ardhi na mirathi .Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa anatembea na wakuu wa Idara wote na Wataalam wake ,baadhi ya mashauri yanatatuliwa hapo hapo mengine anayaelekezwa  mamlaka husika.


Katika hatua zingine Mkuu wa mkoa Amos Makala amewagiza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ,Wajumbe wa Nyumba kumi na Maafisa Watendaji wa Kata Wilaya ya Temeke kuanzisha Ulinzi Shirikishi katika maeneo yao kwa ajili ya kuimalisha ulinzi na usalama katika Kata na Mitaa yao.


Alisema suala la ulinzi ni muhimu na Wajumbe wa Nyumba kumi tushirikiane nao vizuri katika kuimalisha ulinzi inawafahamu watu wote katika maeneo yao.


No comments:

Post a Comment