Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylivester Mwakitalu akizungumza katika Mkutano mkuu wa wa tisa wa Chama Cha waendesha Mashtaka wa Afrika ya mashariki (EAAP) uliofanyika katika Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha.

Naibu karibu mkuu Jumuiya ya afrika ya Mashariki Christopher Bazivamo,akizungumza katika Mkutano mkuu wa wa tisa wa Chama Cha waendesha Mashtaka wa Afrika ya mashariki (EAAP) uliofanyika katika Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha.





Na.Vero Ignatus, Arusha

Mkutano mkuu wa tisa wa chama cha waendesha mashtaka wa Jumuiya ya Afrika ya mashariki (EAAP) umefanyika jijini Arusha ukiwa mikakati ya kubaini,kudhibiti uhalifu dhidi ya Wanyama kwenye makosa yanayovuka mipaka ambapo mkutano huo umebeba kauli mbiu isemayo udhibiti dhidhi ya uhalifu wa wawanyama pori

Mkurungenzi wa Mashitaka nchini Tanzania Sylvester Anthony Mwakitalu amesema Kutokana na maendeleo ya kiteknolojia yaliyopo sasa makosa hayo yana kwenda kuathiri uchumi wa nchi hizo,hivyo kwa umoja wao wameona waje kwa pamoja kuweka mikakati thabiti ya namna ambavyo wanaweza kudhibiti uhalifu.

Amesema kuwa umoja huo umewasaidia kwa kiasi kikubwa kwani uhalifu unapofanyika wanashirikiana kwa pamoja katika kupeleleza,kuendesha mashtaka,sambamba na kubadilishana vielelezo ,ushahidi,pamoja na kuwarejesha watoro waliofanya uhalifu, kutafuta na kutaifisha mali zinzotokana na mazalia ya uhalifu

''Kwahiyo ukifanya uhalifu ukakusanya mali Kenya ukaja kuziwekeza Dar es salaaamzitatafutw apopote zilipo na zitataifishwa kwahiyo tunashirikiana kikamilifu kama kauli mmbiu yetu ya mwaka huu kwamba udhibiti dhidhi ya uhalifu wa wawanyama pori ''Alisema DPP

Amesema kuwa tangia wameanza umoja huo hadi sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa ,Kwani wameweza kuimarisha ushirikiano,ambapo mafanikio hayo yanawaleta pamoja majirani zao, kutoka Malawi,Zambia ,congo,Ethiopia ambapo wanafikiria kuongeza wigo wan chi nyingine

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa waendesha maashitaka jumuiya ya Afrika ya Mashriki (EAAP)nchini Kenya DPP Noorin M.Haji amesema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika mashariki , kwani uhalifu hauheshimu mipaka na inaunganisha nchi nyingine,hivyo ili kudhibiti tatizo hilo hawana budi kuwa na ushirikiano wa karibu

Ameweza kusemakuwa ushirikiano huo umeweza kuzaa matunda waliweza kurejesha dhahabu ambazo ziliweza kuporwa na wahalifu nchini Tanzania ambapo wakenya waliweza kuzirudisha,hivyo waliweza kufanya kwa haraka kutokana na umoja huo ,ikiwepo pia kurejesha wahalifu hatimae waliweza kupelekwa kortini kwaajili ya kusomewa masitaka.

Nae Kimu Mwenyekiti wa umoja huo kutoka nchini Uganda DPP Jane France Obodo ,alisema kuwa umoja huo una faida kubwa kwani wanashirikiana kwa pamoja katika kupambana na uhalifu, kwani unapotoke nchi moja haiwezi kuushuughulikia ipasavyo ,bali kutokana na ushirikiano wao mambo yanakuwa rahisi

Aidha amesema kuwa makosa ya Wanyama pori yanavuka mipaka ,kwani Wanyama waliopo katika hifadhi zao huwa wanahama hivyo wanashirikiana kwa karibu katika kupambana na uhalifu huo.
Share To:

Post A Comment: