Friday, 24 September 2021

MEYA MOSHI JUMA RAIBU AMKOSHA WAZIRI MKUUWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ameendelea na Ziara yake ya kikazi Mkoani Kilimanjaro ya kukagua miradi ya Maendele ya kimkakati ikiwemo Uwekazi wa jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Stand kuu ya Mabasi Moshi, Iliyopo katika kata ya Mufumuni Manispaa ya Moshi.


Wakati wa Uwekaji wa Jiwe hilo la Msingi katika Stendi hiyo itakayogharimu zaidi Shiingi Bilioni 28 (Ishirini na nane) kwa Ujenzi wa stand pamoja na Hotel ya kisasa ua kufikia wageni ya Manispaa hiyo. 


Akihutubia Maelfu ya wakazi wa Moshi, Mh. Majaliwa amesema Mradi huo utakamilika kwa muda kama ilivyoombwa na Mstahiki Meya na wadau wengine.


Katika hotuba yake kwa wananchi Mh. Waziri Mkuu alisema, "Mstahiki Meya nakufuatilia sana, Unafanya kazi nzuri sana, Uko vizuri endelea kusimami fedha za serikali na miradi ya Maendeleo." 


Naye Meya wa Manispaa ya Moshi Mh Juma Raibu alisema yuko tayari kusimamia miradi yote ya Halmashauri bila kumuonea mtu yeyote, Anachotaka ni kazi nzuri yenye thamani ya pesa (Value for Money) nakuhakikishia Mh. Waziri kuwa Hakuna hata mia ya Serikali itakayoibiwa au kudondoka"

No comments:

Post a Comment