Na Elizabeth Joseph,Iringa.


WAWEKEZAJI nchini wameshauriwa kuutumia Mkoa wa Iringa katika uwekezaji kwakuwa ndio lango la Utalii kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pamoja na kuwa Mkoa jirani na Makao makuu ya nchi Dodoma.


Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw,Ibrahim Ngwada wakati akiongea na waandishi wa habari Wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini walikwenda mkoani humo kwaajili ya kutangaza vivutio vya Utalii na Uwekezaji.


Alisema kuwa Mkoa huo umetenga maeneo maalum kwaajili ya uwekezaji ikiwemo Maeneo ya kuegesha magari,kumbi za starehe na mikutano,hoteli,viwanda na majengo ya biashara na kuongeza kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha uwekezaji yanafanyika mkoani humo.


"Uwekezaji katika Mkoa wetu unakua kwa kiwango kikubwa ambapo tayari kwa Upande wa kilimo cha Alizeti,Parachichi,Korosho ambacho uhamasishaji juu ya zao hili ulifanyika na watu wanakaribia kuvuna".Aliongeza Ngwada.


Kuhusu utalii alibainisha kuwa ongezeko la watalii wanatembelea vivutio vilivyopo katika Mkoa huo limeongezeka kwakuwa serikali imeamua kuutangaza Mkoa huo katika sekta hiyo na kuwaomba Watanzania kufika mkoani humo kuona vivutio vilivyopo ikiwemo Hifadhi ya Ruaha,Eneo la Kipongoma alopojiua mama wa marehemu Chifu Mkwawa,Gangilonga kwenye jiwe kubwa linalosema pamoja na maeneo mengine.

Share To:

Post A Comment: