NA HERI SHAABAN


MKUU wa Wilaya Ilala Ng 'wilabuzu Ludigija ametatua mgogoro wa ARDHI Kifuru kata ya Kinyerezi Wilayani Ilala kwa kuagiza Maafisa ARDHI kuhakiki upya eneo hilo na kumaliza changamoto iliyokuwepo zaidi ya miaka kumi


Akizungumza katika kikao cha wananchi Mtaa wa Kifuru Kata ya Kinyerezi Wilaya Ilala Arch, Ludigija alisema kuanzia jumatatu Maafisa ARDHI watahakiki upya eneo na kila mtu atabaki na eneo lake ambalo anamiliki bila kuwekewa vikwazo.


"Wataalam wa Wilaya na Maafisa ARDHI watashirikiana kumaliza mgogoro huu mara moja pale katika changamoto ofisi yangu ipo wazi njooni nitawasaidia kila alhamisi ni siku yenu wananchi ya kusikiliza kero nipo Ofisini na namba yangu mda wote wa kazi ipo wazi " alisema Arch, Ludigija


Arch ,Ludigija aliwataka wakazi wa Kinyerezi  wakiuza maeneo ya ardhi wafuate michoro ya ramani na kujiepusha na mgogoro ya mara kwa mara


Aliwataka wananchi wa Wilaya Ilala wanaponunua ardhi au Mali yoyote wawashirikishe wake zao kwa ajili ya kuja kuwasaidia  .



Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ,Tabu Shaibu ,Maafisa Ardhi,Wanasheria ,Wataalam mbalimbali na wwanasheria



Kwa upande wake Diwani wa Kinyerezi Leah Mgitu  ametoa kilio chake  Serikali kuhusiana na msitu wa Nyuki kwa sasa imekuwa kichaka watu  wanatupwa katika pori  hilo sio msitu wa nyuki hivyo ameomba Serikali kulichukua poli hilo walisafishe libadilishwe matumizi  litumike kwa huduma za jamii 


Diwani Leah ameomba Serikali kuchukua hatua za haraka kulipatia ufumbuzi suala la msitu huo wa nyuki ambalo linahatarisha usalama wa watu na Mali na makazi.


Leah alitaka wananchi wake na Wapiga kura wa Kinyerezi wasisumbuliwe ajalizishwa na kitendo cha Kufungwa kwa akaunti ya mradi wa kurasimisha makazi



Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam Tabu Shaibu amemsimamisha Mkandarasi wa Taka Kata Kinyerezi kwa kukosa sifa ya kazi hiyo akidaiwa kulalamikiwa na wanachi kutokana na huduma yake anayotoa .


Pia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Tabu Shaibu alisema Serikali inatarajia kupandisha hadhi zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha afya changamoto zilizolalamikiwa za zahanati hiyo zinashughulikiwa .

Share To:

Post A Comment: