Jane Edward, Arusha



Baadhi ya wananchi wa kata ya Makuyuni kijiji cha Makuyuni Wilayani Monduli Mkoani Arusha, wanalazimika kutumia nguzo za shirika la umeme Tanzania (Tanesco) kwaajili ya kupata mawasiliano hali inayosababisha kushawishi  wezi wanaohujumu miundombinu ya shirika hilo.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara ya wataalamu wa shirika hilo wananchi hao Justin Lormas alisema vijana wanaoonekana wanapanda kwenye nguzo baadhi yao  wanapanda kwaajili ya kutafuta mawasiliano ya simu kutokana na maeneo yao kutoshika mawasiliano vizuri. 


"Mimi mwenyewe nimeshashuhudia vijana wakiwa kwenye nguzo za umeme, nanilipo wafatilia nikakuta wanatafuta mawasiliano kwenye simu lakini nadhani ni wakati muafaka wa kulinda wahujumu wa miundombinu hii muhimu"Alisema Justin


Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo Afisa usalama Tanesco Arusha John Chirare amesema kuwa  eneo la mita hamsini Kwenye nguzo ni hatari nani makosa Kisheria na kuwataka wananchi kuwasiliana na serikali ili wawasiliane na mamlaka zinazohusika na sekta ya mawasiliano.


"Sisi kama shirika haturuhusu wala kuunga mkono watu kutafuta mawasiliano juu ya minara, hii ni kuhatarisha maisha yao , umeme unaopita kwenye nguzo ni mkubwa"Alisema Chirare


Ametoa wito kwa wananchi kuepuka kujihusisha na matumizi mabaya ya minara hiyo ya umeme iwe kwa kuiba au kufanya shughuli za kijamii chini ya minara hiyo.


Mwisho

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: