Waziri
wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza
kwenye kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja
na kutathmini shughuli za kilimo nchini, leo tarehe 5 Agosti 2021
linalofanyika katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la
Ntyuka Jijini Dodoma.

Afisa
Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la kuendeleza kilimo kusini mwa Tanzania SAGCOT
akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kongamano la saba la wadau
wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo
nchini, leo tarehe 5 Agosti 2021 linalofanyika katika ukumbi wa Asante
Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali
imesema ifikapo Mwaka 2022 itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza
sukari nje ya nchi kwa makampuni ambayo ndio wazalishaji wa ndani wa
bidhaa hiyo.
Upungufu
wa bidhaa hiyo nchini hautokani na uhaba wa miwa bali unasababishwa na
makampuni kushindwa kuongeza uchakataji wa miwa kutoka kwa wakulima.
Waziri
wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 5 Agosti
2021 katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini
Dodoma aliposhiriki katika kongamano la saba la wadau wa sekta ya
kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini.
“Baada
ya mwaka huu Serikali haitotoa vibali kwa wawekezaji waliopewa viwanda
vya sukari kuagiza sukari nje kwani tayari watakuwa wamefikia uwezo wa
kuzalisha sukari toshelevu ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa uanzishwaji
wa viwanda vipya vya sukari hapa nchini”
Waziri
Mkenda amesema kuwa zaidi ya Tani 350,000 za miwa ya wakulima katika
Bonde la Kilombero mkoani Morogoro zinateketezwa kwa moto kutokana na
kukosa soko la uhakika lakini viwanda haviongezi uwezo wa kuchakata miwa
ili kuzalisha sukari ya kutosha.
Amesema
kuwa zaidi ya Tani 40,000 zinaagizwa kutoka nje ya nchi jambo ambalo
sio sahihi kwani viwanda vya sukari vilivyopo nchini vinapaswa kuongeza
uwezo wao ili kuimarisha soko la wakulima jambo litakalopelekea nchi
kutoagiza sukari.
Waziri
Mkenda amesema kuwa mtu yeyote atakayeingiza sukari kiholela ni
wasaliti wa nchi hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amesema
kuwa kuna wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana lakini
viwanda vimeshindwa kuongeza uwezo wake wa kuzalisha sukari ili
kuimarisha sekta ya ajira kwa wananchi.
Katika
mkutano huo Waziri Mkenda ameipongeza serikali na mawaziri
waliotangulia kuiongoza Wizara ya Kilimo kwa kusimamia vyema sekta ya
kilimo ikiwa ni pamoja na kufanikisha kupunguza wimbi kubwa la uagizaji
wa sukari kutoka nje ya nchi.
Post A Comment: