Thursday, 26 August 2021

Naibu waziri wa maji atoa agizo kuondolewa Fundi wa maji Babati

 


Na Mwandishi wetu ,Manyara


NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemwagiza Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Babati Mhandisi Felix Mollel kumuondoa haraka fundi wa miundombinu ya maji anayesimamia mradi wa maji Katika kijiji cha Gidas wilayani Babati, Amos Abi.


Mheshimiwa 

Mahundi amechukua uamuzi huo baada ya kubaini baadhi ya vituo vya kuchotea maji kijijini hapo havitoi huduma kutokana na fundi kutovifanyia matengenezo licha ya kupewa vitendea kazi vyote.


Aidha, ametoa siku tano kwa Meneja wa RUWASA wilayani humo kuhakikisha kasoro zote zilizobainika zinatatuliwa na maeneo yote yanapata maji.


 Vile vile amewataka wataalam wa maji kote nchini waachane na tabia yakukaa ofisini bali watembelea miradi yao ili kubaini changamoto kwa haraka.


Mhe. Mahundi yuko mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi.

No comments:

Post a Comment