Saturday, 7 August 2021

MBUNGE ASIA HALAMGA AZINDUA VIJANA JOGGING KILIMANJARO


Mbunge wa Vitimaalum Kupitia kundi la Vijana Mkoa wa Manyara Asia Halamga amezindua klabu ya Vijana Jogging Mkoa wa Kilimanjaro huku akiwataka vijana wa Chama cha Mapinduzi na Vijana wote wa Mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kushikamana na kufanya mazoezi kwa lengo la kuimarisha afya na kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza leo  wakati wa uzinduzi wa Vijana Jogging Club Mkoa wa Kilimanjrao  uliofanyika  katika mkoani humo.Mbunge Asia Halamga amesema kuwa utaratibu huo utasaidia vijana kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza  pamoja na kuiweka miili yao vizuri.

“Leo tunazindua jogging hii ya Vijana Jogging Mkoa wa Kilimanjro ambayo itakuwa inafanya mazoezi kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi niwatake”amesema Mbunge Halamga

Mbunge Asia Halamga amefanya  mazoezi kuanzia katika Ofisi za Umoja wa Vijana Mkoa wa Kilimanjaro  hadi katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Moshi na Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Vijana Uvccm Mkoa wa KIlimanjaro Ndugu Ivan Mushi,Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo,sambamba na Katinu wa Umoja wa Vijana Uvccm Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Safina Nchimbi.


"Niwaombe muende kuyasimamia haya mazoezi kila mwisho wa mwezi pia tuende tukasimamie afya ili tukajikinge na hili gonjwa nyemelezi,ufanyaji wa mazoezi unaimarisha kinga za mwili hivyo ni wajibu vijana kujikita kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza."Mbunge Halamga

Pia niwaombe na niwatake wananchi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19 ambayo ni ya hiari huku vijana wenzangu muendelee  kufanya mazoezi ili kujikinga na ugonjwa huu.

“Chanjo ni hiari tuhamasishe watu wapate chanjo uhai wa mtu ni yeye mwenyewe wale wenye fursa nendeni mkachanje akili za kuambiwa changanya na zako kikubwa fanyeni mazoezi kujikinga na Corona,” Mbunge Halamga

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro Ivan Mushi amesema wataendelea kuwa mabalozi wa umoja huo wa Vijana kwa kumuunga Katibu Mkuu wao wa Vijana Taifa kwa kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.  


No comments:

Post a Comment