Sunday, 15 August 2021

EAST AFRICAN HEALTH PLATFORM YAZINDUA MPANGO MAALUMU WA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA UGONJWA COVID_19 KWA NJIA YA MTANDAO KWA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

Na Lucas Myovela_Arusha.

lucasmyovela21@gmail.com


Jumiya ya Mashirika ya Afya yasiyo ya kiserikali (East African Health Platform)katika Nchi za Uanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamezindua Jukwaa maalumu la utoaji elimu ya ungonjwa wa Covid_19 kwa njia ya Mtandao kwa wananchi wa Nchi 6 ambazo ni uanachama wa Jumiya ya Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa East African Health Platform (eahp) Dr. Wa Muruchi Kamamia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa mpango maalum wa utoaji elimu ya Afya juu ya ugonjwa wa Covid_19 kwa njia ya mtando kwa Nchi uanachama za Jumiya hiyo,  Mwenyekiti wa East African Health Platform (eahp) Dr. Wa Murichu Kamamia, Ameeleza kwamba mpango huo wa elimu kwa njia ya mtando unalenga kuwasaidia watu wote wa Jumuiya hiyo.

"Katika mpango huu wa utoahi elimu ya Afya  katika Nchi zetu za Afrika Mashariki East African Health Platform (eahp) tumejipanga kuweka mtazamo chanya katika Serikali zetu hasa katika swala zima la Afya pamoja utoaji wa chanjo za Covid_ 19 kwasababu mataifa yetu yanamuingiliano wa karibu na tuapenda kuona hata katika maswala mengine yawe ya umoja". Ameeleza Dr. Wa Murichu.

Aidha pia Dr. Wa Murichu ameeleza kwamba mbali utoa wa elimu hiyo pia wamejipanga vyema katika utoaji wa mafunzo bora ya kiafya kwa watu kuzijua athari za magonjwa husika kwa muda tofauti tofati wa mafunzo ambayo nayo yatafanyika kwa njia ya mtandao ili kutoa fursa ya watu mbali mbali kujijengea uwezo wa elimu ya Afya katika Nchi za uanachama za Afrika Mashariki.

Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa udhani wa East African Health Platform (eahp), Dr Samwel Ogillo

Kwa upande wake Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa udhani wa East African Health Platform (eahp)  ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa Chama cha watoa huduma za Afya Tanzania ( APHFTA), Dr. Samwel Ogillo, Ameelekwamba toka kuanzishwa kwa Jukwaa hilo la East African Health Platform (eahp) waliweza kuongea na viongozi mbali wa Serikali zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki na waliweza kukubaliwa ambapo hivi sasa jukwaa hilo linayo mashirika hamsini 

"Jukwaa hili kazi yake ni moja tu la kutekeleza malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa uzinduzi huu wa Jukwaa la mtandao wa kutoa mafunzo maalum ya Afya kwa watu wote wa Jumuiya yetu wawe madaktari, wauguzi na wengineo watapata mafunzo haya na badae watapata vyeti vitakavyo wasaidia katika kazi zao". Ameeleza Dr. Samwel Ogillo.
Aidha pia Dr. Ogillo ameeleza kwamba changamoto ya ugonjwa wa Covid_19 umethiri kwa kiasi kikubwa muingiliano wa watu wa  Nchi za Jumuiya hiyo kutokana na maambukizi yake kukuwa kwa kasi na kupelekea watu wengi kuto kusafiri kwa shughuli mbalimbali na kuwataka watu wote wa Nchi uanachama kutumia Jukwaa hilo kupata mafunzo bora ya kiafya.
Mwenyekiti msaidizi wa  East African Health Platform (eahp) Dr. Kamamya Mwamulisho.

Mwenyekiti msaidizi wa  East African Health Platform (eahp) Dr. Kamamya Mwamulisho, Ameomba viongozi wa Nchi zote sita zinazo unda Jumiya ya Afrika Mashariki kuangali upya sera ya vipimo na utoaji wa chanjo za ugonjwa wa Covid_ 19 ziwe za Juiya nzima ili kupunguza msongamano kwa kila Nchi kuwa na taratibu zake.

"Ugonjwa wa Covid_19 umesimamisha shuguli nyingi za watu, Wito wangu kwa serikali zetu zote kama zinaweza kuungana kwa kuwaruhusu watu waliyo fanyiwa vipimo vya Covid_19 katika Nchi yake vipimo hivyo vikubaliwe katika Nchi nyingine ya Jumuiya yetu". Amesema Dr. Kamamya Kamulisho.

"Aidha niwaombe viongozi wa Serikali zetu kama wanaweza kusaidia kununua chanjo kwa wananchi wao ili kupunguza gharama za upatikanaji wa chanjo ya Covid_19, Pia ikiwezekana tupate dawa ya aina moja itakayo tumika kwa Jumuiya yetu maana ugonjwa huu umeathiri uchumi wa Nchi zetu sote". Dr. Kamamya Mwamulisho.

No comments:

Post a Comment