Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James  akizungumza na Wananchi wa kata ya Saranga waliojitokeza katika mkutano wake wa kusikiliza kero za Wananchi katika Mtaa wa Temboni
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wilaya hiyo namna ya kushughulika na kero za Wananchi

Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika Mkutano wa Mkuu wa Wilaya wa kusikiliza kero za Wananchi uliofanyika katika mtaa wa Temboni ikiwa ni Mkutano wa kwanza wa Mkuu wa Wilaya hiyo katika kusikiliza kero za Wananchi.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amewapongeza wananchi wa kata ya Saranga na Ubungo Kwa ujumla kwa kazi nzuri katika kusimamia shughuli za Miradi ya maendeleo pamoja na kujipanga vizuri katika Suala la Ulinzi na Usalama.

DC James amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Saranga kabla ya kuhitimisha ziara yake katika kata hiyo na kutamka kuwa swala la ushirikiano Kati ya wananchi na Serikali ni muhimu ili Ubungo yetu iwe salama.

" nawapongeza wenyeviti wa mitaa kwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwenye Mitaa yenu. Ili kuhakikisha Ulinzi na Usalama unaimarika kwenye Mitaa yetu ni vema kila mmoja mwenye uwezo wa kufanya kazi awe na shughuli ya kufanya na Serikali tutahakikisha tutatengeneza mazingira bora ya kumwezesha kila mtu kufanya kazi badala ya kujihusisha na uhalifu"Amesema DC James.

Aidha DC James alitoa tahadhari juu ya suala la usafi na mazingira kwa kusema kuwa Kuna magonjwa mengi yanasababishwa na uchafu, Napenda Ubungo iwe mfano Kwa kuwa na barabara na maeneo ya wazi Safi, kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, niwasisitize watendaji kuzingatia usafi na tuache tabia ya kutupa taka ovyo, pandeni miti ili kuweka Wilaya yetu Safi ukizingatia Wilaya yetu ndio lango la jiji  

"Serikali inaleta fedha nyingi za miradi ni wajibu wenu wananchi kuilinda na kuitunza, vilevile jengeni utamaduni wa kutembelea miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yenu ili kuifahamu lakini pia kutoa taarifa kama kuna changamoto yoyote mapema" Amesema DC James.

Amesema kuwa serikali inatoa Elimu bila malipo kama wazazi mtaamua kuchangia fedha ili watoto wasome masaa ya ziada hayo ni makubaliano yenu na kwa wanafunzi watakaoshindwa kuchangia wasilazimishwe hiyo ni ziada sio lazima.

Aidha DC James ametoa wito kwa wananchi hayo juu ya Janjo ya UVIKO 19 na kuwataka kuachana na uvumi ulioenea kuwa chanjo inapelekwa kwenye shule na inazua taharuki kwa wanafunzi wakiona gari kwenye mazingira ya shule, napenda kutoa maelezo kuwa hicho kitu hakipo na hakiwezi kutokea kwani chanjo ni hiari ya mtu. 

Aidha katika Wilaya yetu tunatarajia kwa na siku mbili za kutoa chanjo eneo la wazi ili wale wanaotaka kuchanja na wanakosa muda wapate huduma hiyo.



Share To:

Post A Comment: