Na Woinde Shizza , ARUSHA 


Baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wamewalalanikia wasomaji mita za maji wa  mamlaka ya maji Safi na maji taka Arusha (AUWASA ) kuwazidishia bili za maji pindi wanapokwenda majumbani

Waliyasema hayo juzi wakati walipokuwa wakiandamana kuelekea Katika ofisi za mamlaka hiyo ambapo walisema kuwa julio chao kikubwa kulichowafanya waandamane ni kwenda kulalamikia tatizo la bili kuletewa bili kubwa za maji za maji tofauti na matumizi yao.   
 Akiongea na waandishi wa habari Moja wa wananchi hao Joseph John Mkazi wa mbauda Jr alisema kuwa  wasomaji mita ndio tatizo tatizo kubwa kwani  wamekuwa wanasoma mita lakini wanavyoenda kupiga mahesabu wanatuma majibu tofauti na walivyosoma mita.

"Mfano mimi walivyokuja kunisomea mita ilikuwa inasoma nimetumia unit 26 lakini walipoenda uko ofisini kwao wamenitumia bili inayoonyesha nimetumia unit 47 kitu ambacho sio cha kweli  mimi nimezoea kulipa bili elfu 9000 Sasa wanavyoniletea bili ya efu 44000 kwa mwezi wanategemea nini mimi nalipaje "alibainisha John

Alibainisha kuwa alipofika idara ya maji kutoa malalamiko walimsikiliza nakumwambia   hilo ni tatizo la kibinadamu na watalifanyia kazi na atarudia kulipa bili Kama awali alivyokuwa analipa.

Alitoa wito kwa uongozi wa AUWSA  kuwapa elimu ya kutosha wasomaji mita kwani kwa asilimia kubwa wanaonekana awana elimu ya kutosha,huku aliwataka kuhakikisha wanapokwenda kusoma mita  wahakikishe wapo na mwenyeji ambaye atahakikisha jinsi walivyosoma na kuandika ni ukweli ili malalamiko yapungue

Neema Raphael  mkazi wa moshono aliwataka AUWSA kutoa elimu kwa wananchi juu ya elimu ya usomaji mita pia aliwataka wasome bili kwa usahihi na pia kuwepo na ushirikishwaji baina ya wafanyakazi wa mamlaka ya maji na wananchi.

Akiongelea swala hilo mkuu wa kitengo na mahusiano ya umma kutoka mamlaka ya maji Safi na maji taka (AUWSA) Masoud Katiba alisema kuwa  amepokea malalamiko hayo lakini  sio ya kweli kwani wao kama AUWSA wamekuwa wakiwashirikisha  wateja wao usomaji mita  na Kama wengine wakiwakuta hawapo wamekuwa waki tumiwa bili zao kwa njia ya ujumbe mfupi wa  simu (sms).

Alisema kuwa swala la kuzidishiwa wa bili linatokana na matumizi ya mteja jinsi anavyotumia maji ndivyo jinsi anavyoletewa bili inavyokuja ,pia alisema kuwa bili kuwa kubwa kunatokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuvuja kwa bomba upande wa mteja  yaani mbele ya mita .

Alisema kuwa  wametenga dawati la huduma  kwa wateja linaloshulikia kero kwa ajili ya wateja wao ambapo mbali na hilo dawati hilo limekuwa kutembelea wateja wao kwa ajili ya kukagua miundombinu ya maji ya wateja.
Share To:

Post A Comment: