Jane Edward, Arusha


Hali ya taharuki imezuka katika kata ya sokoni 2  halmashauri ya Arusha baada ya wananchi kuchoma moto nyumba ya mkazi  wa sokoni 2 ,Ng'ida Loisulye kwa madai ya kubomoa nyumba ya ndugu yake ,Benjamin Mollel  ambayo bado kesi ilikuwa mahakamani.



Aidha wananchi hao walifikia hatua ya kuchoma moto nyumba ya mkazi huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ametumia ubabe kufanya tukio hilo kwani hakuna oda yoyote ya mahakama iliyotolewa ya kuvunja nyumba hiyo kwani kesi bado ipo mahakamani na hakuna hukumu yoyote iliyotolewa.



Wakizungumzia tukio hilo ,wahanga waliobomolewa nyumba hiyo, Benjamini Mollel alisema kuwa,anashangaa kuona polisi wamefika nyumbani kwake wakiwa na madalali ambao walifika kubomoa nyumba hiyo hali ambayo walikuwa hawana taarifa yoyote kuhusu kubomolewa kwa nyumba.


"mimi nina kesi na huyu ndugu yangu muda mrefu na tulishapelekana kuanzia ngazi za chini hadi imefika mahakamani na tulishaweka kuzuizi nyumba isibomolewe na kesi ilikuwa inatajwa tena septemba 6 ,mwaka huu Sasa nashangaa leo wamefika hapa kuja kubomoa wakati hatuna barua wala taarifa yoyote kuhusu tukio hili."amesema Benjamini.




Naye Diwani wa kata hiyo ya sokoni 2,Obedi Melami alisema kuwa, yeye alikuwa nyumbani kwake na kupigiwa simu kuhusu taarifa za kubomolewa kwa nyumba hiyo ndipo alipofika eneo la tukio na kukuta   nyumba hiyo ikibomolewa.


"mimi nimeshangaa sana tukio hilo kuja kufanyika bila kuwepo kwa taarifa yoyote kwa Mtendaji wa kata,kijiji na hata mimi pia sikuwa na taarifa yoyote maana matukio kama haya ni lazima tupate barua ya kushirikishwa kisheria tukiwa kama viongozi  wa kata ili tuweze kusimamia kwa umakini zaidi,lakini nashangaa sijui kilichofanyika."amesema Diwani huyo.

Share To:

Post A Comment: