Tuesday, 27 July 2021

Tanzia : Afisa Elimu wilaya ya Babati afaridi dunia kwa ajali.

 

Kwenye picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati John Nchimbi

Na John Walter-Babati

Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari (Afisa elimu) wilaya ya Babati Paulina Mpare, amefariki dunia kwa ajali ya gari baada ya gari alilokuwa anasafiria kupasuka tairi na kuacha njia eneo la Makutupora mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati John Nchimbi amethibitisha kifo hicho na kueleza kuwa Mpare alikuwa akirudi Babati akitokea Dar es Salaam alipokuwa akimuuguza ndugu yake.
Nchimbi amesema taarifa alizozipata kutoka kwa wasamaria wema zinaeleza kuwa afisa huyo alifariki dunia julai 26 majira ya jioni akiwa mapokezi katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma alipofikishwa ili kuokoa uhai wake.
'Alipatiwa msaada na wasamaria wema katika gari kampuni ya Shabiby' alieleza Nchimbi
Amesema Mpare alikuwa ni kiungo muhimu katika ukuaji wa taaluma katika Halmashauri ya wilaya.
Kuhusu taratibu za mazishi,Nchimbi amesema wanasubiri utaratibu wa familia.

No comments:

Post a Comment