Saturday, 10 July 2021

SERIKALI YATOA UFAFANUZI IDADI KUBWA YA WAGONJWA WA CORONA ARUSHANaibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel amesema asilimia kubwa ya wagonjwa waliofikishwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakihofiwa kuambukizwa corona hawana tatizo hilo bali wanasumbuliwa na magonjwa mengine ya mfumo wa hewa.

DkMollel ameyasema hayo baada ya kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kujionea hali ambapo amesema kati ya wagonjwa 44 waliokuwa na matatizo ya kupumua ni wanne tu wamethibitika kuwa corona na wengine wana matatizo mengine yenye dalili zinazofanana na corona.


Aidha Dk. Mollell amewataka watendaji wa sekta ya afya na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari zote za kukabiliana na janga la corona kwani tatizo lipo.

No comments:

Post a Comment