Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza  siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato cha sita 2020/2021 kushoto ni Mwalimu wa Taaluma Msaidizi wa Shule ya Sekondari Coastal High Shool Moses Mhina
Mwalimu wa Taaluma Msaidizi wa Shule ya Sekondari Coastal High Shool Moses Mhina akizungumza wakati wa mkutano huo kushoto ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete
Mwalimu wa Michezo na Klabu za Jamii kwenye shule  hiyo akieleza namna michezo inavyochangia ufaulu kwa wanafunzi Salim Mwakumuna kushoto ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete
Sehemu ya walimu wa shule ya Sekondari Coastal High School wakiendelea na majukumu yao kama walivyokutwa
Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete akikagua madaftari ya wanafunzi kama inavyoonekana


SERIKALI imeshauri kuweka juhudi kubwa kuwezesha vifaa vya kufundishia ambavyo vitasaidia kuwa na wanasayansi halisi kwa kusoma kwa vitendo ili kuweza kuendana na uchumi wa viwanda.

Hayo yalisema na Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Coastal High School, Isaack Dastan Kifwete wakati mkutano wao baina yao na waandishi wa habari uliokuwa na lengo la kueleza  siri iliyowafanya kung’ara kwenye matokeo ya kidato cha sita 2020/2021..

Shule hiyo imefanya vizuri katika matokeo hayo  baada ya Wanafunzi kuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza na Pili tu (Division I na II)yaliyopatikana shuleni hapo na kuifanya kuwa ya kwanza katika wilaya ya Tanga.

Alisema matokeo hayo yamewawezesha kuendelea kuwa shule ya kwanza(Namba 1)katika wilaya ya Tanga mjini huku wakiwa shule ya nne(Namba 4) kwa mkoa wa Tanga.

Aidha alisema mafanikio hayo yamechagiwa na uongozi pamoja na walimu walio bora ikiwemo kujituma bila kuchoka na wanafunzi kuwa na ari katika masomo.

"Kwanza ni ushirikiano kutoka kwa Mkurugenzi wa Shule hii Mathew Marupa kuwa na walimu bora na wanajitoa kwa muda wote hali hii imesaidia kuwezesha kupata matokeo mazuri”Alisema

Alisema pia ni kuwekwa kwa bidii kwenye masomo wanayosimamia pamoja na kuwa na wanafunzi wanaojitambua ambapo pale wanapofika wanapewa malengo ya shule kuwa hautakiwi kufeli unapokua kwenye shule hii"alisema Kifwete.

Aidha alisema kwa miaka minne mfululizo shule hiyo imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora ya kujifunza na hivyo kupelekea kuelewa kila wanachofundishwa.

Awali akizungumza katika mkutano huo,Mwalimu Msaidizi wa Taaluma Moses Mhina ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Sayansi anafundishi masomo ya Kemia na Biologi alisema matokeo ya kidato cha sita wanakuwa wakifanikiwa kutokana na uwepo wa nidhamu ya hali ya juu ambalo kwao ndio jambo la kwanza kabla ya taaluma.

Alisema wanafunzi wanapofika shuleni jambo la kwanza ni nidhamu,la pili ni ushirikiana kati ya walimu na wafanyakazi wengine,kujitoa ni jambo ambalo ni kubwa sana kwao na wakati mwengine kufanya kazi nje ya muda wa kazi na kuwafundisha wanafunzi kwa waledi ambao unawatengenezea ujasiri.

“Lakini pia ushirikiano walimu na watu wa nje ambao sio walimu hasa wazazi na walezi kwa sababu kunaweza kutokea changamoto ya utoro lakini tunapokutana na wazazi na kuwaeleza utoro unavyokwamisha matokeo mazuri na hivyo wao kutupa ushirikiano “Alisema

Alisema siri nyengine ambayo imewasaidia wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kufanya vizuri ni kuwatengenezea mtazamo chanja unajua kwenye malezi wanayolelewa mtu tangia akiwa mdogo anasikia habari kwa kaka zake kwamba sayansi ni ngumu lakini wao wanafunzi wanapofika shuleni wanawaelezwaa namna wanavyuoweza kufanya masomo hayo bila woga na hivyo kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo .

Mwalimu huyo alieleza kwamba hatua inayoondolea woga kwao na hivyo kuwajengea namna ya kujiamini na kumtengeneza ujasiri wa kujibu maswali na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri wanapokuwa kwenye mitihani yao.

“Lakini pia tumekuwa tukifanya ziara ya kutembelea kwenye viwanda na hivyo kuona namna sayansi inayoweza kufanya kazi na hivyo kuwawezesha wanafunzi kupata uelewa mpana “Alisema

Hata hivyo pia siri nyengine ni wao kujitahidi kufundisha kwa waledi na kutoa mazoezi ya kutosha kwa wanafunzi yanayowapa ujasiri wa kutambua mambo mengi na hivyo kuwawezesha kutimiza ndoto zao za kufanya vizuri.

Mwisho

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: