Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela,amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima sambamba na kuendelea kuchukua tahadhari ya   ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kuvaa barakoa na  kunawa mikono  kwa sabuni na maji tiririka.

Mhe.Mongela ameagiza hayo wakati wa ziara yake  ya siku moja  Wilayani Arumeru ya kukagua mashamba ya mazao ya mbogamboga, maua, matunda na viungo kwa lengo la kuona uhalisia wa uendeshaji wa mashamba hayo.

Aidha, amesema   Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuhakikisha  sekta zote za kiuchumi zinakuwa na tija.

Mhe.Mongela amesema baada ya kutembelea mashamba hayo siku ya Kesho atakua na kikao na wadau wa Kilimo cha mazao ya mbogamboga, matunda na maua ili kuhakikisha sekta hiyo inafanya vizuri.

Ziara hiyo ilijumuisha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi wa TAHA na Maafisa wengine wa Serikali ambapo mashamba 6 yalitembelewa.

 

Share To:

Post A Comment: