Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau akizungumza na Wanawake wa Umoja wa chama hicho  (UWT) Mkoa wa Singida katika Kongamano la kutathmini Siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani pamoja na mafanikio ya wanawake hapa nchini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye kongamano hilo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Shee akizungumza kwenye kongamano hilo.

Wanawake wa CCM wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wanawake wa CCM wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.

Maombi ya kifanyika kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.

Maombi yakiendelea.

Maombi ya kifanyika kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.

Wanawake wa CCM wakiwa kwenye kongamano hilo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida Jane Kessy akizungumza kwenye kongamano hilo.

Katibu wa UWT Mkoa wa Singida, Edina Kugulu akiongoza kongamano hilo.

Kongamano likiendelea.

Mbunge Martha Gwau akivikwa vazi la kimila kwenye kongamano hilo.

Mbunge Martha Gwau akikabidhiwa kibuyu cha kimila wakati wa kongamano hilo.
Martha Gwau akiwa amejitwisha kibuyu hicho baada ya kukabidhiwa. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida Diana Chilolo.

Afisa Utumishi wa CCM Makao Makuu Dodoma, Veronica Ndalo akizungumza kwenye kongamano hilo.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi akizungumza kwenye kongamano hilo.

Kongamano likiendelea.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Lusia Mwiru akizungumza kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Victolina Ludovick akizungumzia mafanikio ya sekta ya afya mkoani hapa.
Mtaalamu wa masuala ya afya kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Abdallah Balla akizungumzia ugonjwa wa Corona na namna ya kujikinga nao.
Mratibu wa CHF iliyoboreshwa wa Manispaa ya Singida Doristas Seveline akizungumzia ubora wa mfuko huo pamoja na jinsi ya kujiunga.
Kongamano likiendelea.
Kongamano likiendelea.


Dotto Mwaibale, Singida. 

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Singida  Martha Gwau ametoa bima za afya kwa wanawake 400 mkoani hapa ili ziwasaidie kupata matibabu.

Gwau alitoa bima hizo jana wakati akihutubia kwenye kongamano la wanawake Mkoa wa Singida lililofanyika Ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma ambapo pamoja na mambo mengine walitafakari siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwa madarakani na mafanikio ya wanawake hapa nchini huku kauli mbiu ikiwa ni ‘Wanawake ni Nguzo ya Maendeleo’ Kaziiendelee.

” Bima hizi  ni  zawadi ya Afya kutoka katika mfuko wa ofisi yangu na nijuhudi za kumuunga mkono Rais wetu
Samia Suluhu Hassan katika kuboresha afya za akina mama kwani bila afya hakuna maendeleo na ili maendeleo yaje na kufanya kazi kwa bidii ni budi kila mtu kuwa na afya njema, hivyo nimeamua kugharamia suala la afya kupitia mfuko wa bima wa CHF kwa wanawake hawa ambao ni sawa na kaya 400 huku wanufaika wakiwa 2400 pamoja na watu wenye uhitaji maalumu
“.alisema Gwau.

Alisema bima hiyo itakuwa  ya watu sita kutoka kwenye kila familia ya wanawake hao 400.

Gwau alisema mwaka huu ameanza na kaya 400 lakini matarajio yake ni kufikisha kaya 1000 na wanufaika wakiwa zaidi ya 5000 itakuwa vizuri zaidi na anafanya hivyo kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwatumikia watanzania katika sekta ya afya.

Pia Gwau alisema kuanzia kesho atatoa utaratibu kwenda kwenye halmashauri zao ambako anatoka kila mwanamke kwa ajili ya kujisajili ambapo wanatakiwa watu sita yaani baba, mama na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18.

 Gwau alitumia kongamano hilo kwa ajili ya kuwashukuru wanawake hao kwa kumchagua kwa kura nyingi na kuwaomba ushirikiano ambapo pia alieleza mipango na mwelekeo wake wa kazi za maendeleo mkoani Singida.

Alisema ataanza ziara zake za kikazi katika wilaya zote na kata ili kwa pamoja waweze kutatua kero za wanawake huku
vipaumbele vyake vikiwa ni kuwainua wanawake kiuchumi na kuwapatia elimu na mafunzo mbalimbali na kuijenga Jumuiya yao ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) 

Alisema katika masuala ya kuwasaidia wanawake atakuwa akifanya kwa awamu kulingana na atakavyo jaliwa lakini ya
kiutendaji yatakuwa wilayani ambapo aliwaomba wamshike mkono, wamuelekeze, wamshauri na kumkoasoa lengo likiwa ni kuijenga Singida.

Aidha Gwau aliwaomba wanawake hao kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ni mwanamke wa kwanza hapa nchini kushika wadhifa huo mkubwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambapo alisema kwa umoja wao wanapaswa kuonesha mshikamano na jinsi walivyo tayari kufanya naye kazi akiwa katika nafasi hiyo na kumuombea kwa Mungu.

Katika hatua nyingine aliwataka wanawake hao kuchangamkia fursa ya kilimo cha alizeti kwa kuwa ndio zao kubwa la
biashara mkoani hapa na Serikali imeweka nguvu ya kulilima kwenye  mikoa mitatu ya Singida, Dodoma na Simiyu.

Pia aliwaomba  madiwani wanawake kusimamia na kuwashauri wanawake kuchangamkia mikopo kutoka katika halmashauri zao kwaajili ya kujiletea maendeleo na kuinua uchumi wa mwanamke.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Singida Alhaji Juma Kilimba ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kongamano hilo alimshukuru Gwau kwa kuandaa kongamano hilo na kuwashukuru wanawake hao kwa kumchagua kuwa mbunge.

Aliwataka wanawake hao kuwa wamoja na kushirikiana kwa kila jambo sambamba na kuimarisha jumuiya yao ili chama hicho kiendelee kuongoza nchi.

Katika kongamano hilo Gwau aliwaalika wataalamu ambao walitoa mada kuhusu masuala ya afya hususani namna ya kujikinga na ugonjwa wa corona na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya.

Share To:

Post A Comment: