Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida amekabidhi  rasmi Ofisi  kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango.

Muro  amewashukuru Viongozi wa Halmashauri za Arusha na Meru, Kamati ya ulinzi na Usalama, Watumishi wa Wilaya hiyo na Viongozi wa Dini na Mila na Wananchi kwa Ushirikiano waliompa kipindi cha uongozi wake na kuwataka kushirikiana na Mkuu  mpya wa Wilaya .

Naye Eng.Richard Ruyango,Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru ambaye ametokea katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ametoa dira ya Wilaya kuwa itajikita katika ushirikiano wa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ili kuharakisha Maendeleo Wilayani humo.

Eng.Ruyango ameeleza kuwa ataendeleza Yale mazuri yaliyopo Arumeru ambapo amewataka Watumishi kuchapa kazi  kwa bidii na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Serekali katika suala la maendeleo.

Aidha, Wakuu hao wa  Wilaya wamemshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwaamini na kuahidi kumwakilisha vyema kwa kutatua changamoto za Wananchi na kusimamia shughuli za Maendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Marcuz Nazi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi amewapongeza Wakuu hao wa Wilaya kwa kuendelea kuaminika na kuteuliwa katika nyazifa hizo pia ametumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Eng.Richard Ruyango, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  na kumuaga Mhe. Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro (Kushoto) akimkabidhi  rasmi  Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango(kulia).

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Ndg.Jerry Muro Mkuu wa Wilaya ya Ikungwi akiagana na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Mkurugenzi Mtendaji WA Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmmanuel Mkongo wakati WA Ukaribisho WA Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.





Share To:

Post A Comment: