Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen ameendelea na ziara yake ya  kuzungumza na wenyeviti wa matawi na mashina pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.

Katika ziara hiyo Zelothe alitembelea na kujionea ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa kukagua vyoo vya wanafunzi wakike vyenye matundu 12 vilivyogharimu Milioni 16,900,000 Halmashauri ya Arusha Dc ikichangia Milioni 13,200,000 huku michango ya wananchi milioni 3,700,000 katika shule ya Msingi Kata ya Kiranyi yenye wanafunzi 1260 na walimu 25.


“Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa vyoo hivi vya watoto wetu wa kike kwa kuwa vimejengwa kwa umakini na vimeweza kutumia fedha zilizotolewa na Serikali ipasanyo,niwapongeze walimu,Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hii kwa kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii.''Alisema Zelothe
 
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha Neema Mollel amepongeza mradi huo unaotekelezwa na Halmashauri ya Arusha Dc kwa kuwa na ubora unaotakiwa kutokana na dhamani ya pesa ambayo imetumika katikaujenzi huo.

"Halmashauri wamefanya kazi kubwa kuhakikisha wanazitumia fedha za wananchi vizuri kwa kutekeleza ahadi za kutengeneza miradi kwenye ubora wake kulingana na dhamani ya fedha ambayo imetolewa kwenye mradi husika." Alisema Neema Mollel











 

Share To:

Post A Comment: