Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, Ndg Geoffrey Kirenga akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU)  wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Mrajis Mkuu wa Vyama Vya Ushirika Tanzania Dkt Benson Ndiege akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) tarehe 28 Juni 2021, uliofanyika katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Moshi

Serikali imeonyesha kutoridhishwa na muenendo wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) ambapo wanachama wametakiwa kusimama imara wakati wa uchaguzi katika kuhakikisha wanapatikana viongozi bora ambao wataiwezesha KNCU kusonga mbele.

Taarifa ya tume ya waziri Mkuu kuhusu KNCU imebainisha madudu mengi ambapo baadhi ya mali mbalimbali zilihujumiwa na nyingine kuuzwa ikiwemo kuingiwa kwa mikataba isiyo sahihi.

Kati ya vyama vya ushirika 43 vilivyofanyiwa ukaguzi na shirika la ukaguzi wa mahesabu kwa vyama vya ushirika (COASCO), vyama 12 vimepata hati zisizoridhisha jambo ambalo halileti taswira nzuri.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo tarehe 28 Juni 2021 wakati akizungumza kwenye mkutano mkuu wa 36 wa chama kikuu cha ushirika Mkoani Kilimanjaro (KNCU) ambapo amesisitiza kuwa serikali inahitaji sheria hiyo ifanyiwe marekebisho ili kuiwezesha kuleta tija kwenye ushirika.

Amesema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kufanya marekebisho ya sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013  lengo likiwa ni kuondoa madhaifu yanayodidimiza vyama hivyo nchini.

Waziri Mkenda amewataka wanaushirika kuipitia sheria hiyo na kutoa maoni ambayo yatawezesha kuiboresha sheria hiyo na kuifanya kuwa na tija katika vyama vya ushirika nchini.

"Ingekuwa ni mamlaka yangu ningesema viongozi wote wa bodi waondoke na msigombe na tuchague wengine ila kwasababu ushirika ni mali ya wanaushirika niwaombe mtumie nafasi yenu kuhakikisha mnawashawishi wale wenye uwezo kugombe nafasi za uongozi" Amesema Waziri Mkenda na kuongeza kuwa

"Kwa hali hii naona vyama vya ushirika vishindane  katika kupata hati safi maana ni lazima hesabu zipangwe vizuri maana mali bila daftari huisha bila habari"

Aidha, Prof  Mkenda aliutaka umoja wa vyama 32 vya ushirika (G32) kufuata sheria kama wanavyopewa maelekezo na Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini, katika kuanza kufanya biashara ya kahawa na kwamba iwapo watashidwa kufuata sheria serikali haitakuwa radhi nao.

Akizungumza katika mkutano huu, Mrajisi wa Taifa wa vyama vya ushirika, Dkk Benson Ndiege, amesema mkutano Mkuu wa uchaguzi wa KNCU uliahirishwa kwa lengo la kutoa frusa kwa wanachama kuchagua  viongozi Bora ambao watakuwa na uwezo na ubunifu.

"Tatizo kubwa linalokabili vyama vya ushirika hapa nchini ikiwa ni pamoja na KNCU Ni kukosekana kwa dhana ya utawala bora, mkutano wa uchaguzi umeahirishwa tumieni nafasi hii kupata viongozi ambao wataitoa KNCU ilipo na kuisogeza mbele kwa manufaa ya wakulia" Amesema

Naye Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika Kahama (KNCU), Emanuel Cherehani, amesema ili KNCU ifanikiwe ni lazima viongozi kuwa waaminifu, waadilifu pamoja wabunifu ili kusaidia chama hicho kupiga hatua zaidi na wakulima kuona mchango wake.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, Ndg Geoffrey Kirenga amesema kuwa KNCU ina nafasi kubwa kurudisha heshima ya Ushirika Tanzania.

Share To:

Post A Comment: