Na Lulu Mussa Dodoma.


Waziri   wa   Nchi   Ofisi   ya   Makamu   wa   Rais   (Muungano   na   Mazingira)   Mhe.Selemani   Jafo  amewaagiza   wamiliki   wa   kumbi   za   starehe   na   burudani kuhakikisha sauti zitokanazo na shughuli zao hazizidi viwango vinavyokubalikakwa mujibu wa sheria.


Waziri Jafo amesema hayo hii leo Jijini Dodoma wakati wa kutoa Tamko kwaumma juu ya udhibiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kelele na mitetemona kuwaagiza wamiliki wa maeneo ya burudani na starehe kuzingatia matumizi ya vipima kelele na vizuia sauti kama ilivyoelekezwa kwenye masharti yote ya leseni zao.


“Katika kuhakikisha tunalinda Afya ya Jamii kutokana na athari zitokanazo nakelele   na  mitetemo   Ofisi   ya   Makamu   wa   Rais-Muungano   na   Mazingira,   kwakushirikiana   na  Ofisi  ya   Rais   –   TAMISEMI;   Ofisi   ya   Waziri   Mkuu   Uwekezaji;Wizara   ya   Afya,   Maendeleo   ya   Jamii,   Jinsia,   Wazee   na   Watoto;   Wizara   yaViwanda na Biashara;  Wizara   ya   Ardhi   na   Maendeleo   ya   Makazi;   Wizara  yaElimu, Sayansi na Teknolojia; Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; na Wizara yaHabari,   Sanaa   na   Michezo   tunaelekeza   Kila   Mwananchi   ahakikishe   shughulianazofanya hazisababishi kero ya kelele na mitetemo” Jafo alisisitiza.


Aidha, Waziri huyo amesema kasi ya ukuaji wa uchumi inaenda sambamba naongezeko la shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambazo zinaambatanana ongezeko la uchafuzi wa mazingira unaotokana na Kelele na Mitetemo nakusababisha athari za kiafya na kimazingira kwa jamii.Aliongeza kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika Nyanja zakiuchumi   na   kijamii   kutokana   na   Mipango   madhubuti   ya   Serikali   kwenyeUwekezaji katika Sekta mbalimbali.


Hivyo,   ameutaka   umma   wa   Watanzania   kuhakikisha   agenda   ya   kelele   namitetemo inakuwepo kwenye mikutano ya wakazi na kuwaomba wananchi kutoataarifa kuhusu kero na mitetemo kwa Ofisi za Serikali za Mitaa au NEMC kwaNamba za bure (0800110115 au 0800110117 au 0800110116)Amesema   yeyote   atakayesababisha   kero   zitokanazo   na   kelele   na   mitetemokinyume na Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa kelele na mitetemo)za mwaka 2015 atakuwa amevunja sheria na adhabu yake ni faini isiyopunguashilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miezi sita, sambamba na kufungiwakwa biashara husika.


Kwa   upande   mwingine   Waziri  Jafo   ametoa   rai   kwa   viongozi   wa   Dini   kupitia Kamati za Amani, kulijadili suala hili la Kelele na Mitetemo iliyopitiliza kutoka kwabaadhi ya nyumba za  ibada ili   kupata  namna   bora  ya   kuendesha  ibada  kwamaslahi mapana ya afya ya jamii.


Nae Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. DorothyGwajima   amesema   wataendelea   kuelemisha   jamii   juu   ya   athari   za   kiafyazitokanazo na kelele na mitetemo iliyopitiliza ili kuwa na jamii yenye afya bora nakupunguza gharama za matibabu kwa Serikali.


Waziri Jafo aliambatana na Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia na WatotoMhe.   Dorothy   Gwajima,   Naibu   Waziri   wa   Ardhi,   Nyumba   na   Maendeleo   ya Makazi  Mhe. Angelina Mabula,  Naibu Waziri Ofisi  ya  Waziri Mkuu WenyeUlemavu Mhe. Ummy Nderiananga; Naibu Waziri Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia Mhe. Omary Kipanga; Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani yaNchi Mhe. Khamis Chillo; na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul

Share To:

msumbanews

Post A Comment: