Meneja urasimishaji Ardhi Vijijini  wa MKURABITA Athon Temu akitoa mafunzo juu ya Urasimishaji Ardhi na Matumizi ya hati miliki za kimila kwa wakulima wa Chai wa Wilaya ya Kilolo

Baadhi ya wakuli wa Chai walioshiriki katika Mafunzo ya Siku moja juu ya Urasimishaji Ardhi na Umuhimu wa kuwa na hatimiliki za Kimila kwa lengo la kuzitumia ili kujiongezea Kipato.

 

 NA JOSEPH MPANGALA -IRINGA

Zaidi ya shilingi Billion 25.8 zimetolewa na Taasisi za Kifedha na kwenda kwa wakulima waliotumia Hati za Kimila kama dhamana na kufanikiwa kukopa na kuendeleza mashamba  pamoja na Biashara katika Urasimishaji uliofanywa katika  Halmashauri 54.

Hayo amesemwa na Meneja M Urasimishaji Ardhi Vijijini  wa MKURABITA Athon Temu alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku moja kwa Wakulima wa Chai wa wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa tayari kwa ajili ya kupata Hati miliki za kimila kwa Vijiji Vitano.

“Mkurabita kwa kurasimisha hatuangalii tu Kupata hati lakini matumizi yake ya kiuchumi namna gani inakwenda kukuinua wewe kiuchumi wewe na faminia yako ukaongeza mapato kwa maana ya mtu mmoja mmoja mapato yako yakiongezeka basi mapata ya taifa yataongezeka”amesema Temu.

Aidha Mafunzo hayo yameshirikisha wakulima wa Chai Kutoka Vijiji vya Kidabaga,Ilamba,Lusimba,Magome pamoja na Ndagasiwila.

Meneja urasimishaji Ardhi Vijijini  wa MKURABITA Athon Temu akitoa mafunzo juu ya Urasimishaji Ardhi na Matumizi ya hati miliki za kimila kwa wakulima wa Chai wa Wilaya ya Kilolo. Baadhi ya wakuli wa Chai walioshiriki katika Mafunzo ya Siku moja juu ya Urasimishaji Ardhi na Umuhimu wa kuwa na hatimiliki za Kimila kwa lengo la kuzitumia ili kujiongezea Kipato.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na MKURABITA.

 

Share To:

Post A Comment: