Aliyekuwa Rais na mpigania Uhuru wa nchi ya Zambia Hayati Kenneth Kaunda alikuwa rafiki mkubwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kupelekea mataifa yote kuwa rafiki na kuleta maendeleo ya watu.


Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Uhamasishaji Chipuki wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Ally Mohammed Ummy mara baada ya kufika katika Ubalozi wa Zambia nchini Tanzania kwaajili ya kutoa salamu za rambirambi kufuatia kwa msiba wa Hayati Kenneth Kaunda uliotokea hivi karibuni.


Amesema wao kama vijana wa CCM wamepkea kwa masikitiko kwasababu wameridhi historia ya nchi rafiki ya Zambia na Watanzania na matokeo yake   yanaonekana baada ya kuwepo kwa miradi ya maendeleo.


"Urafiki wao ndio ambao ulipelekea kuishawishi taifa la China kuweza kujenga reli ya TAZARA ambayo kwa mara ya kwanza ilitambulisha nchi ya China katika mataifa ya Afrika katika nyanja za uhandisi na kupelekea nchi ya China badala yake kuaminiwa katika zabuni mbalimbali na kuongeza mahusiano ya kidiplomasia na nchi za Afrika". Amesema Bw.Ummy.


Aidha Bw.Ummy amesema Hayati Mwalimu Nyerere na Kenneth Kaunda waliangalia katika karne ya 20 ni namna gani wanaweza kubadili dhana ya mataifa yao na watu wake kutoka katika dhana inayoegemea katika misingi ya kikabila kuja katika dhana ambayo inajielekeza katika Uchumi wa Maendeleo ya watu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: