Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitunduweta wilayani Kilosa, Thomas Lukoo akieleza mafanikio na changamoto za biashara ya mkaa wanazokumbana nazo katika kipindi cha utekelezaji wa mradi mbele ya Wataalamu wa habari kutoka Taasisi za Serikali,Mashirika yasiyo ya kiserikali na halmashauri za wilaya waliokwenda kujifunza kuhusu mradi huo kijijini hapo.
Meneja wa mradi wa kuleta mageuzi katika sekta ya mkaa Tanzania (TTCS) Charles Leonard akieleza jitihada wanazozichukua katika kukabilia na changamoto mbalimbali  ambazo zinakwamisha jitihasa za mradi na wadau wake.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCG) Emmanuel Lyimo akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo na maswali yaliyojitokeza kwenye majadiliaono hayo kati ya Wataalamu hao wa habari na wanakikundi katika kijiji cha Kitunduweta.
Mafunzo yakiendelea.
Afisa Mazingira kutoka NEMC kanda ya kati bwana Kawa Kafuru akieleza aliyojifunza kwenye ziara hiyo ya siku moja kwenye kijiji cha Kitunduweta.
Wataalamu wa masuala ya habari na mawasiliano,maafisa wa mradi pamoja na wanakijiji cha Kitunduweta wakishiriki mazungumzo hayo kabla ya kwenda msituni kuona kazi zinazofanyika.
Wataalamu wa masuala ya habari na mawasiliano,maafisa wa mradi pamoja na wanakijiji cha Kitunduweta wakishiriki mazungumzo hayo kabla ya kwenda msituni kuona kazi zinazofanyika.
Wataalamu wa masuala ya habari na mawasiliano,maafisa wa mradi pamoja na wanakijiji cha Kitunduweta wakishiriki mazungumzo hayo kabla ya kwenda msituni kuona kazi zinazofanyika.


Na Calvin Gwabara, Morogoro.


WADAU wa Misitu hasa Wananchi wenye mfumo wa uhifadhi shirikishi wa misitu ya vijiji wameiomba Serikali kuangalia upya tamko lake la GN 417 kwakuwa linakwamisha jitihada za uhid]fadhi wa misitu yao na kuhamasisha uharibifu Zaidi kwenye maeneo ambayo hayana usimamizi huo wa misitu nchni.

Wito huo umetolewa na Mtendaji wa Kijiji cha Kitunduweta kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho kilichopo wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, Thomas Lukoo ambao wanashiriki na kunufaika na usimaizi shirikishi wa mistu ya kijiji chao kwa muda wa miaka mitano sasa toka waanze kufanya kazi na Mashirika ya TFCG na MJUMITA.

”Tangazo hilo la Serikali limeathiri sana mfumo wetu wa usimamizi wa mistu ya kijiji na motisha ambayo kijiji chetu na hata vijiji vingine vilivyo kwenye mfumo huu kwani GN 417 imetoa bei elekezo ya gunia la mkaa la KG 50 nchi nzima kuwa shilingi 12,500 bila kuzingatia ubora wa mkaa wenyewe na umbali mkaa huo unakotoka na hivyo kuwafanya wateja wasije kwenye vijiji vyetu na kuishia maeneo ya karibu ambako wanaupata kwa urahisi na hivyo hawaji kwetu na hivyo kukimbilia kwenye vijiji avya jirani ambavyo havina utunzaji wa misitu” alisema Lukoo.

Amesema hapo awali Kijiji kilikuwa kinapata mapato mengi kwakuwa walikuwa na uwezo wa kuchoma mkaa kwenye vitalu 83 kwa mwaka kwakuwa wateja walikuwa wanafuata mkaa unaochomwa kihalali na kwa kufuata vibali lakini kwa mwaka huu wamevuna kwenye vitalu 20 pekee na hivyo kusababisha ile motisha ambayo wanakijiji wamekuwa wakiipata kupitia uchomaji mkaa kupungua kwa kiasi kikubwa.

Mtendaji Charles Lukoo amesema kupitia mfumo huo wa ulinzi shirikishi wa misitu wamefanikiwa kulinda msitu wa kijiji chao vizuri na kuzuia uharibifu mkubwa ambao ulikuwa ukifanyika huko nyumba kabla ya mradi huo kuanza hasa baada ya kuona motisha za moja kwa moja kwa vijiji na Wananchi kupitia miradi ya maendeleo na hivyo kuona kazi ya kulinda misitu sio ya serikali pekee bali ni jukumu lao.

Akizungumzia changamoto hiyo Meneja wa Mradi wa kuleta mageuzi kwenye sekta ya mkaa Tanzania  (TTCS) bwana Charles Leonard amesema GN 417 imeathiri sana jitihada kubwa zilizofanywa na wadau, Mradi na Wananchi katika kulinda misitu hiyo kwani inashusha ari ya wananchi kutokana na zile motisha walizokuwa wanazipata kupungua kwa kiasi kikubwa.

Meneja huyo wa mradi amesema jitihada mbalimbali zimefanywa na wadau wote kwenye mradi katika kuona namna Serikali inavyoweza kufanya marekebisho ya tangazo lake na ikiwezekana Tangazo hilo lisiguse vijiji ambavyo vinavuna mkaa na mazao mengine kwa njia endelevu na wapewe uwezo wa kupanga bei inayofaa kwa maslahi mapana ya Misitu,Vijiji na Taifa.

“Sisi kama mradi katika kukabiliana na changamoto hii na athari zake tumeanza kufikiria mbinu zingine mbadala katika mfumo huo katika ngazi za vijiji kwa kuzungumza na vijiji kuona namna ya kupunguza fedha kidogo inayoingia kwenye kijiji katika kila gunia ili kumpatia mchomaji kama motisha ili kuwavutia wawee kuendelea na kufanya biashara hiyo ingawa bado utaratibu wa awali ulifaa zaidi“ Alisisitiza meneja wa mradi bwana  Charles.

Mradi wa kuleta mageuzi kwenye sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) unatekeleza dhana ya uendelevu wa misitu ya vijiji na kulinda Mazingira nchini unatekelezwa na shirika la la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa jamii usimamizi wa misitu Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la uswis (SDC).

Mradi huu unatekelezwa kwenye vijiji 30 kwenye vilaya ya Kilosa,Mvomero, na Wilaya ya Morogoro Mkoani Morogoro kwa kutumia mfumo bora wa usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii (USMJ) ambao unatoa matisha kubwa katika vijiji na kuboresha maisha ya wananchi kwa kujenga miundombinu ya shughuli mbalimbali muhimu za kijamii kwenye vijiji.

Share To:

Post A Comment: