Mkuu wa Wilaya ya Karatu akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Monduli ACP Edward Balele.
Vijana wa Skauti wakimvika Skafu ya Heshima Mkimbiza Mbio Maalum za Mwenge Kitaifa Luteni Josphine Mwambashi mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Monduli mapema hii leo akitokea katika Wilaya ya Karatu.

Muonekano wa Mradi uliokataliwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.

Na Imma Msumba, Monduli

Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru mapema hii leo umendelea kuchanja mbuga Mkoani Arusha  kwa kuendelea kuzindua miradi mbalimbali,kuweka mawe ya msingi, kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Monduli huku kauli mbio ikisema  “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu.''

Mapema hii leo Wakimbiza Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa wamekataa kuzindua mradi wa kufyatua matofauli wa halmashauri ya Monduli kutokana na dosari mbalimbali ikiwemo kutoridhishwa na fedha zilizotumika kwenye ujenzi wa majengo mawili ya mradi huo,kutokamilika kwa nyaraka za mradi pamoja na kutokuwepo kwa mikataba ya wafanyakazi huku wafanyakzi wakitishwa wanapodai stahili zao.

Pamoja na hapo Kiongozi wa mbio Maalum za Mwenge Kitaifa Luteni Josphine Mwambashi amezitaka Halmashauri za majiji,manispaa na wilaya kuacha urasimu usiokuwa na sababu katika kutoa malipo ya kazi zinazofanywa na vikundi vya vijana ambavyo vimeanzishwa kwa fedha za mikopo ya asilimia 10 yanayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Ameyazungumza hayo kiongozi wa wakimbiza mwenge maalumu wa uhuru Luteni Josephine Mwambashi wakati akizundua mradi wa vijana wa Monduli mkoani Arusha wa kutengeneza bidhaa zitokanazo na chuma ya kiwemo Madirisha,Madawati,Milango,Viti na meza nadhamani mbalimbali za ndani.

Awali kabla ya kuzinduliwa kwa mradi huo wa Vijan Mwenyekiti wa kikundi hicho cha five Star welding chenye uwekezaji wa shilingi milioni 16 Frank Kaaya amebainisha mbele ya Kiongozi wa mbio maalum za Mwenge Kitaifa kuwa kikwazo kikubwa kinachowakabili kwa sasa ni ucheweleshaji wa malipo huku wakidai shilingi milioni 2.9 kwa halmashauri ya Monduli na hivyo kuwakwamisha kuendelea kufanyakazi nyingine ya ujenzi wa maabara ya moja ya shule ya sekondari.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli Steven Ulaya akaahidi kulipa deni hilo kabla ya Jumatatu ijayo ambapo kiongozi huyo wa mbio za mwenge Luteni Josephine Mwambashi amekataa na kuagiza malipo ya vijana hao yafanyike kabla ya Mwenge wa Uhuru  kuondoka hapo kesho kwenye Wilaya yaMonduli.

Mwenge huo umepita katika miradi 9 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 394.3 ikiwemo ya kilimo cha umwagiliaji mbogamboga JKT Makuyuni,Mradi kusafisha na kutibu maji ya mabwawa yatokanayo na mvua,Mradi wa Duka la Dawa katika Hospital ya Monduli pamoja na mradi wa kufwetulia matofali ambapo haukuzinduliwa kutokana na sababu zilizopo.

Share To:

Post A Comment: