Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewataka wabunge wanaotokana na Jumuiya ya wanawake Tanzania (UWT) kusimamia kwa karibu utolewaji wa fedha za mikopo ya wanawake katika Halmashauri zote nchini.


Ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao cha Kawaida Cha Baraza Mkuu la UWT lililofanyika katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama Dodoma leo tarehe 26 Juni, 2021.


"Wabunge wa UWT wote, wakae waandike taarifa kwenye kila maeneo yao wanapotoka au mkoa kuhusu asilimia nne (4%) ya fedha za Halmashauri walivyozisimamia na zilivyoleta tija katika eneo hilo kwa wanawake, lakini na namna walivyowasilisha kwenye vikao vyao ngazi ya wilaya na mikoa ili kuleta muunganiko na usimamizi wa karibu wa fedha hizi."


Aidha, pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu ametoa msisitizo kwa viongozi wote wa UWT kuweka mkazo katika kukutana na kufanya vikao kuanzia ngazi za matawi walipo wanachama na wananchi na ajenda ya kudumu iwe ni fursa za wanawake, ukilinganisha na ngazi zingine ambapo vikao uhusisha viongozi pekee.


Imetolewa na;

Said Said Nguya

Afisa Habari

Ofisi ya Katibu Mkuu

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Share To:

msumbanews

Post A Comment: