Mshauri wa Mkuu wa Shirika na Katibu wa Sheria wa Shirika la Umeme la TANESCO  Wakili Amosi M.Ndegi kulia akimkabidhi vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya watoto Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo   Bi.Beatrice Rimoy  katika halfa iliyofanyika leo Hospitalini hapo vufaa hivyo vina thamani ya Milioni 4
Mshauri wa Mkuu wa Shirika na Katibu wa Sheria wa Shirika la Umeme la TANESCO  Wakili Amosi M.Ndegi kulia akimkabidhi vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya watoto Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo   Bi.Beatrice Rimoy  katika halfa iliyofanyika leo Hospitalini hapo vifaa hivyo vina thamani ya Milioni 4

Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo   Bi.Beatrice Rimoy  kushoto akiangalia vifaa tiba alivyokabidhiwa leo na Mshauri wa Mkuu wa Shirika na Katibu wa Sheria wa Shirika la Umeme la TANESCO  Wakili Amosi M.Ndegi  kwa ajili ya wodi ya watoto Hospitalini hapo vifaa hivyo vina thamani ya Milioni 4
Mshauri wa Mkuu wa Shirika na Katibu wa Sheria wa Shirika la Umeme la TANESCO  Wakili Amosi M.Ndegi akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya Milioni 4
Sehemu ya Msaada ambao ulitolewa

SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO leo wametoa msaada wa vifaa tiba kwenye wodi ya watoto kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo vyenye thamani ya Milioni 4 kwa ajili ya kuwasaidia watoto.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo na Mshauri wa Mkuu wa Shirika na Katibu wa Sheria wa Shirika la Umeme la TANESCO  Wakili Amosi M.Ndegi,kwa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali hiyo  Bi.Beatrice Rimoy

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Wakili Amosi alisema wameona ipo haja ya kutoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto kwenye hospitali  hiyo ikiwa ni sehemu yao ya kurudisha kwa jamii.

“Tumeona ipo haja ya kutoa msaada huu wa vifaa tiba kwa watoto kwenye hospitali hii kama sehemu ya kurudisha kwa jamii na tunaimani vitatumika kama ilivyokusudiwa”Alisema

Alisema kwa kawaida  shirika hilo limekuwa na utamaduni wa kufanya mkutano ya Kiidara au watu wenye taaluma moja wanaofanya kazi pamoja kwenye shirika kipindi hiki wapo Tanga wao  kama Idara ya Ukatibu wa Sheria inayohusisha wanasheria na maafisa usalama wa Shirika hilo lengo ni kufanya tathimini ya malengo waliokuwa nayo katika utendaji wa shughuli za kawaoda za kila siku kwenye shirika hilo mwaka mzima.

“Tupo hapa Tanga wiki nzima tukijadili mafanikio na changamoto ili kupata namna nzuri ya utendaji kuboresha huduma inayotolewa na shirika la Umema Tanzania kwa jamii watu wengi wanadhani TANESCO  ni Shirika la Kibiashara ,lakini hapana tupo kuhuduma zaidi na ndio maana leo tupo hapa tukiwezesha huduma ya watoto Hospitalini lakini pia hata bei ya Umeme vijijini sasa ni elfu 27000,badala ya laki tatu (300,000) na hii pia ipo kihuduma zaidi kuhakikisha wananchi wote wanamudu gharama za kuunganisha Umeme"Alisema
 
Alisema pia wanaziangalia changamoto zinazowakabili ili kutafuta majibu na utatuzi wake kwa lengo la kurahisisha na kuboresha mazingira na hari kwa watendaji walionao.

“Lengo letu kubwa kuwepo hapa ni kwamba tulikuwa na jukwaa la Idara ya Katibu wa Shirika,ambayo hukutana   kila mwaka kuzungumzia tathimini na changamoto za utendaji kazi zetu ndani ya Shirika,na kwa kuhitimisha kikao chetu leo, TANESCO  kama sehemu ya jamii   tumeona ipo haja ya kutoa msaada wa vifaa tiba kwa watoto Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo “Alisema

Awali akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Afisa Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Beatrice Rimoy amelishukuru Shirika la Umeme nchini Tanesco kwa msaada huo ambao ulikuwa ni uhitaji mkubwa wa watoto .

Alisema na mahitaji yao yamegawanyika kwenye maeneo matatu ikiwemo watoto wadogo sana waliozaliwa chini ya mwezi mmoja ,waliozaliwa ambao hawajafika umri wa mwezi mmoja,wana wodi ya watoto wa mwezi mmoja mpaka miaka 10 ikiwemo watoto wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo ya kuambukiza , kuharisha na matumbo hivyo msaada huu ambao utasaidia kuwahudumia watoto hao.

Naye kwa upande wake Daktari wa wodi ya watoto kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Dkt Tumaini Mchiiyo- amelishukuru shirika hilo kwa kuwapa vifaa ambavyo vitawasaidia sana watoto wenye changamoto mbalimbali na hivyo kuwezesha watoto kupata tiba iliyoboreshwa zaidi wawapo hospitalini

Mwisho
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: