Mkuu wa TAKUKURU-ARUMERU Bwana Deo Mtui (kushoto) akikabidhi kiasi cha Tshs.7,000,000/= kwa maafisa mapato wa Halmashauri ya Meru kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya MERU.

Afisa wa TAKUKURU-ARUMERU Bwana Athanas Kimumbi (kulia) akikabidhi kiasi cha Tshs.300,000/= kwa mwananchi mnyonge aliyekuwa amedhulumiwa na Mwajiri wake kiasi cha Tshs.1,000,000/=

MKUU WA TAKUKURU wilaya ya ARUMERU Bwana Deo Mtui akiwakabidhi Maafisa Mapato wa Halmashauri ya Meru fedha za Ushuru wa Usafi wa Mazingira kiasi cha Tshs.6,000,000/= ambazo zilikuwa zimechepushwa na kampuni ya Usafi na Mazingira iliyokuwa imepewa tenda ya kukusanya ushuru huo.
Jackline Kapileh Afisa MWANDAMIZI wa TAKUKURU-ARUMERU(kushoto) akikabidhi kiasi cha Tshs.1,300,000/= kwa Afisa Mapato wa Halmashauri ya Meru.
Afisa wa TAKUKURU-ARUMERU Bi. Hadija akimkabidhi Mtumishi wa idara ya fedhaHalmashauri ya Meru kiasi cha Tshs.5,200,000/= zikiwa ni fedha za Ushuru wa Usafi na Mazingira ilizokuwa inaidai kampuni iliyokuwa imepewa tenda ya ukusanyaji wa ushuru huo na ikawa haiwasilishi makusanyo YAKE kwa wakati kwa mujibu wa sheria na makubaliano.

Wananchi wa Wilaya ya Arumeru wanaendelea kunufaika na kasi ya utendaji ya  Taasisi ya KUZUIA na  KUPAMBANA na  RUSHWA  Wilayani humu ambapo  TAKUKURU kwa kipindi cha mwezi Februari na Machi 2021 imeweza kuokoa mamilioni ya fedha na kurejesha chache zilizohitajika kwa haraka kiasi cha Tshs.19,800,000 ambapo kati ya fedha hizo Tsh 19,500,000/=  ni fedha za USHURU wa Usafi na Mazingira za  Halmashauri ya Wilaya ya Meru.


Na Kiasi cha Tshs.300,000/= ni fedha za  Mwananchi Mnyonge aitwaye Anate Nanyaro ambaye alikuwa amedhulumiwa na Mwajiri wake kiasi cha Tshs.1,000,000/= 


Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya ARUMERU  Ndg. Deo Mtui amesema  fedha hizo za USHURU wa Usafi na Mazingira,  kiasi cha Tshs.19,500,000/=

zimetolewa kwa awamu nne (4) 

ambazo zilikabidhiwa kwa maafisa mapato wa Halmashauri ya MERU, Emiliana Julias, Neema Mollel, Sigfrid Janga na Mabuye kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru Ndugu EMMANUELI MCONGO.


Ambapo, awamu ya kwanza tarehe 28/02/2021 kilikabidhiwa  kiasi cha Tshs 7,000,000/=, awamu ya pili, Tarehe 03/03/2021, kiasi cha Tshs.6,000,000/=, kiasi kingine cha Tshs.5,200,000/= kilikabidhiwa tarehe 09/03/2021 na awamu ya nne, kilikabidhiwa tarehe 12/03/2021 kiasi cha Tshs.1,300,000/=,  sambamba na fedha kiasi cha Tshs 300,000/= alizodhulumiwa mwananchi mnyonge aliyekuwa na shida ya haraka ya kutatua.


Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya ARUMERU, Bwana Deo Mtui amesema TAKUKURU Wilayani Arumeru imejipanga kuhakikisha Wananchi wote  waliodhulumiwa ndani ya wilaya ya ARUMERU kwa namna yoyote ile wanapata haki yao kwa wakati sambamba na  kudhibiti ubadhirifu na ufujaji wa fedha za umma kwa uthubutu wa kutokumvumilia mtu yeyote.


Mtui ametoa wito huo  kwa Wananchi wote waliodhulumiwa haki zao na  ambao wameshindwa kuzipata haki hizo  kwa wakati wasisite kufika TAKUKURU ARUMERU na kwenye ofisi mbalimbali za TAKUKURU nchi nzima ili wapatiwe haki zao.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: