Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema Wahandisi wa halmashauri nchini wanaongoza kwa kuikosea serikali kwa kushauri vibaya kitaalam katika miradi ya ujenzi kwa kuweka gharama za juu zaidi hali inayopelekea kutokukamilika kwa miradi mingi kutokana na kutokufuta bajeti inayopangwa na serikali kuu.


Naibu waziri Silinde amesema hayo baada ya kutembelea miradi ya ujenzi wa mabweni katika halmashauri za Bariadi na Itilima mkoa wa Simiyu na kukuta haujakamilika huku wakilalamikiwa wahandisi kwa kutoa makisio ya bei za juu ya ujenzi kuliko hali halisi ya ujenzi.


"Nimepita katika halmashauri zingine gharama ile tuliyotoa ya milion 80 imemaliza ujenzi kwa kuwa baadhi ya wakuu wa shule walibana matumizi na kusimamia vizuri fedha walizopewa. Lakini katika maeneo mengine wengi walioshindwa kumaliza walifuata ushauri wa wahandisi wasio wazalendo kwa serikali yao ambao uliwapotosha na kuweka gharama kubwa zaidi na kufanya walimu kuingia matatizoni kwa matumizi mabaya ya fedha hali iliyopelekea kuwasimamisha nyadhifa zao" 


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga amemuahidi naibu waziri Silinde kuwa mpaka ifikapo mwezi wa tano majengo yote ya mabweni yatakuwa yamekamilika kwa fedha za ndani baada ya fedha walizoletewa na serikali katika shule mbili wilayani kwake kwa ujenzi wa mabweni milion 160 kushindwa kumaliza majengo hayo.


Katika hatua nyingine Naibu waziri Silinde amewaagiza wakuu wa shule za Itilima sekondari, Bariadi sekondari,Nyasosi sekondari na maafisa elimu sekondari wilaya ya Bariadi na Itilima kuandika barua ndani ya siku ya kwa nini wamechelewa kumaliza ujenzi kwa wakati na lini watakamalisha ujenzi huo na endapo watashindwa kukamilisha majengo hayo kwa muda walioomba kuongezewa basi atawavua nyadhifa zao.

Share To:

Post A Comment: