Mh.Waziri akimtwisha ndoo mmoja wa wananchi wa kijiji cha kashangu Halmashauri ya Itigi mara baada ya kuzindua mradi huo.


Waziri na watendaji wa RUWASA pamoja na Viongozi wengine wa Wilaya ya Manyoni wakipanda juu ya Tanki la maji linalohudumiwa na mradi wa kintinku.

iongozi akiwemo Pius Chaya katikati wakiongozana na Mh.Waziri kutoka kwenye chanzo cha maji katika mradi wa kintinku Wilayani Manyoni..
Waziri akiteta jambo na Meneja wa RUWASA Mhandisi Lucas Said.

Mh.Waziri akizungumza mara baada ya kukagua chanzo cha mradi wa kintinku Wilayani Manyoni.



 Na Mwandishi wetu,Singida.


WAZIRI wa Maji,  Jumaa Aweso ametoa siku saba kwa Meneja wa wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini na mijini (RUWASA) Mkoa wa Singida kumlipa Mkandarasi anayejenga mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Kintinku Wilayani Manyoni.

Aweso alitoa kauli hiyo juzi wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani hapa ya kutembelea miradi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo ya maji.

Baada ya Waziri kujionea utekelezaji mzuri wa mradi huo unaojengwa na Mkandarasi mhandisi Jumanne Werema kutoka kampuni ya (CMG)ambaye anadai zaidi ya shilingi milioni 700 huku mradi ukiwa katika hatua za mwisho Waziri akaagiza ndani ya wiki ijayo Mkandarasi huyo awe amelipwa fedha hiyo.

"Naagiza RUWASA Mkoa mlipeni huyu Mkandarasi fedha yake,haiwezekani Mkandarasi amefanya kazi nzuri namna hii na mradi umekamilika alafu asilipwe hela yake.Meneja mlipeni ndani ya wiki ijayo." alisema Aweso.

Aidha Aweso amempongeza Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Manyoni mhandisi Gabriel Gongi kwa kuokoa shilingi milioni 150 katika ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Kashangu katika Halmashauri ya Itigi ambapo mradi huo umegharimu shilingi milioni 200 badala ya 350 kabla ya kutumia mfumo wa Force Account.

"Nakupongeza sana Meneja,hawa ndio Viongozi tunaowataka,umekuwa mwaminifu ungeweza kufanya vyovyote lakini kwa uzalendo ukatumia kiasi hiki. Hiyo pesa iliyobaki ikatumike sehemu nyingine ambapo mnaona kuna changamoto zaidi lengo letu ni kumtua mwanamke ndoo kichwani." na kuongeza.

"Hapo nyuma miradi ilikuwa inatumia gharama kubwa wakati wa kutekelezwa lakini kwa sasa watendaji wengi wamebadilika hongereni sana,hayo ndio Mh.Rais anayataka kuyaona. na wiki ya maji mkoa wa Singida tutazindua zaidi ya miradi 10 ya maji haya ni mafanikio makubwa." alisema Aweso


Hata hivyo aliwaomba wananchi wanaozunguka maeneo ya miradi kuilinda na kuitunza miradi hiyo ambayo imetumia pesa nyingi za Serikali ili iwasaidie  kwa sasa na hata vizazi vijavyo.

Awali akizungumza na wafanyakazi wa idara hiyo Aweso aliwapongeza kwa ushirikiano ambao umepelekea mafanikio makubwa ndani ya wizara na kusema kuwa lengo ni kuona kati ya wizara tatu zitakazo tajwa kuwa zimefanya vizuri wizara ya maji iwe miongoni.

"Ndugu zangu tufanye kazi kwa ushirikiano tuache songombingo..tubadili mitazamo, tufanye kazi usiku na mchana ili Wananchi wapate huduma bora


Share To:

Post A Comment: