Tuesday, 23 February 2021

TAKUKURU fanyeni uchunguzi ujenzi wa bweni shule ya Sekondari Kitama

 


Na. Mwandishi wetu TANDAHIMBA

Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. David Silinde amemsimamisha kazi mkuu wa shule ya sekondari ya Kitama katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, Mkoani Mtwara kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa mabweni moja na matumizi mabaya fedha. 

Ametoa uamuzi huo  wakati akikagua ujenzi wa miundombinu ya  shule hiyo ambapo shilingi bilioni milioni  78 zimetumika katika ujenzi wa bweni  na kufikia hatua  ya upauaji huku Halmashauri nyingine zikitumia gharama hizo na wameweza kukamilisha ujenzi huo, fedha ambazo zilitolewa na serikali kupitia mradi ya lipa kwa matokeo EP4R.

Mhe Silinde ameiagiza Taasisi ya kuzuia rushwa Takukuru katika Mkoa huo  kuhakikisha wanachunguza matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo kwa kuangalia  thamani ya pesa alizotumia katika ununuaji wa vifaa na ujenzi.

Katika hatua nyingine Mhe. Silinde amemuagiza Afisa elimu sekondari Sosteneth Luhende kuandika barua ya kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu na kuvuliwa madaraka baada ya kushindwa kusimamia  ujenzi wa mradi huo na kutobana matumizi.

"Nimetembelea Halmshauri ya Longido nimekuta wamemaliza ujenzi wa  mabweni manne kwa gharama ya milion 320 ambapo kila bweni moja limejengwa kwa gharama ya shilingi milion 80 na yamekamilika , ikiwemo miundombinu ya maji, kule ni mbali tofauti na hapa ambapo vitu ni bei nafuu lakini cha ajabu hapa mmenunua vitu gharama ya juu, bila kubana matumizi angalia tu hata ujenzi wenyewe unatia mashaka” amesema Mhe. Silinde

Ameendelea kusema kuwa uchunguzi wa kina ufanyike ili kujua thamani halisi ya fedha iliyotumika, nondo zilizowekwa ukilinganishwa na BOQ ilivyokuwa  ili kujirizisha na matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa na Serikali.

 


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema wamepokea maelekezo ya Mhe Silinde ameiagiza  ofisi ya TAKUKURU kuanza  uchunguzi wa gharama zilizotumika za ujenzi shuleni hapo.

Katika kujitetea, Mkuu wa shule ya Kitama Twaha Chitipu amesema changamoto waliyopata wakati wa utekelezwaji wa mradi wa bweni hilo mpaka kuchelewa kukamilika ilikuwa ni upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli za ujenzi ambapo na kuchelewa  kwa makubariano ya eneo kati ya mwenyenalo na shule ili kuruhusu ujenzi wa bweni

No comments:

Post a Comment