NAIBU waziri wa maji(MB) Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wananchi wa Kijiji cha Mwabaratulu katika halmashauri ya wilaya Kwimba Mkoani Mwanza kutunza miundo mbinu ya maji ili serikali ifikie malengo yake sambamba na kumtua mwanamke ndoo kichwani .


Mhandisi Mahundi amesema kuwa wanawake ndo wahanga wakubwa wa tatizo la maji ikiwa ni pamoja na kuwepo na migogoro katika ndoa.


Naibu waziri Mahundi amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Mwabaratulu wilaya ya Kwimba mradi.ulioghalimu shilingi milioni .177.


"Mheshimiwa Rais Magufuli ametoa fedha nyingi katika miradi ya maji nchini hivyo wataalamu na wananchi tunapaswa kushirikiana ili kuifikia matamanio ya Rais kuona kila Mtanzania anakunywa maji safi na salama" amesema Mhandisi Mahundi.


Hate hivyo Naibu waziri ametoa ofa ya mwezi mmoja kwa  wananchi wa kijiji hicho  kutumia maji bure bila malipo.


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: