Monday, 1 February 2021

MNEC KUBECHA AWATAKA VIONGOZI WA CHAMA KUSIMAMIA KIKAMILIFU UTEKELEZAJI WA ILANI;Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa anayetokana na kundi la Umoja wa vijana awayasema hayo leo wilayani Siha wakati akufungua darasa la Itikadi na Siasa ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM.


Mnec Kubecha baada ya kufungua darasa la Itikadi na Uongozi alielekea katika kukagua miradi ya vijana ambapo alitembelea Green House ya miche ya nyanya iliyoundwa na vijana wasiopungua 100 kutoka katika kata mbalimbali za wilaya ya Siha,


Pamoja na hilo lakini pia aliagiza umoja wa vijana kisaidia kuanzishwa kwa vikundi vya vijana katika kila kata, Alikwenda kutembelea Ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM wilaya ambapo aliendesha harambee na kupatikana mifuko 60 ya saruji ambapo aligawa mifuko hiyo kwa viongozi wa UVCCM wilaya ya Siha.


MNEC KUBECHA alikwenda mbali zaidi pale alipo washukuru wadau wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine ujenzi huo na kuwaomba waendelee kufanya hivyo ili kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huo.


MNEC alikemea tabia ya dharau,chuki,fitina na uhasama miongoni mwa viongozi wa kisiasa na kuwaomba kudumisha umoja,upendo,mshikamano na maridhiano katika kushughulika na changamoto za wananchi huku akisisitiza kuwa uchaguzi umekwisha wananchi wanataka matokeo ya ahadi tulizowaahidi


"Muda wa ahadi umekwisha,huu ni wakati wa matokeo ya ahadi tulizowaahidi wananchi wakati wa kampeni. Wananchi wanaimani na serikali ya CCM hivyo ni wajibu wetu kufanya kazi na kuacha maneno maneno,fitna,chuki na uhasama." Mnec Kubecha


"Kila mmoja aonyesho ubora na uimara wake kwenye kazi,Unapomhujumu mtu fulani asifanye kazi kwa sababu ataonekana,Atakuzidi huo ni ushamba na ujinga,Huwezi kuonekana  kwa kuzuia wengine,huwezi kuwa imara kwa kubomoa wengine,Huwezi kuwa bora kwa kuwachafua wengine."


"Chama ndicho kinachoiongoza serikali,Chama kinatoa maelekezo na kuisimamia serikali,Sio serikali kukisimamia chama ama viongozi wa serikali kukiamuru chama."


Imetolewa na

Katibu Hamasa Wilaya Ya Sih.

No comments:

Post a Comment