Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amesema kuwa kazi ya kuunganisha umeme ni popote ulipo tutakuletea umeme.


Dkt.Kalemani ameyasema hayo Februari 17, alipokua akiongea na wananchi wa kata ya Bwongela na 

Muganza, alipokwenda kukagua kazi ya usambazaji umeme inayoendelea katika vitongoji hivyo.


"haijalishi nyumba yako ni ya nyasi, udondo au ya bati, sisi popote utakapo kuwepo tutakutundikia umeme" alisema Dkt. Kalemani


Aidha amewataka wananchi wote ambao hawajafanya "wiring"wafanye ili waweze kuwekewa umeme na kusisitiza TANESCO nchi nzima kuwafungia umeme wateja waliokwisha kulipia umeme ndani ya Siku 30 na kununua pikipiki ili ziweze kutumiwa na 'saveyors' kuepuka usumbufu wawatu kukaa muda mrefu bila kufanyiwa tathmini ya gharama wanazotakiwa kulipa. 


"Na hili ni agizo kwa TANESCO nchi nzima muwanunulie ma saveyor bodaboda, waweze kufanya kazi kwa kasi tunayoitaka" amesema Dkt.Kalemani


Vile vile amewataka wananchi ambao tayari wameshapata umeme kuutumia umeme kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindikaji mazao na mashine za kusaga na kukoboa ili matunda ya umeme yaonekane katika vipato vyao.

Share To:

Post A Comment: