1.      MkuuwaMkoa wa Singida Dtk. RehemaNchimbi katikati akiongoza Kongamano la Fursa za Uwekezaj ikwenye Mkoa wa Singida, Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Lucy Sheen,  kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi.

Wakuu  waWilaya zaMkoawaSingida(kwenye mstari wa kwanza) wakifuatilia Mada mbalimbali wakati wa Kongamano la uwekezaji Mkoani Singida.



1.    

1.

1.    Viongozi wa Wachimbaji Madini Mkoa wa Singida wakiwa kwenye banda lao wakionyesha madini mbalimbali kwa wadau waliotembelea banda  la wachimbaji wa madini Mkoa wa Singida (SIREMA).


Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakionyesha bidhaa zao

  • RAS ASEMA MKOA UMEJIANDAA KIKAMILIFU

 

Na John Mapepele, Singida

 

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe, Dkt. Rehema Nchimbi  amewataka  Wawekezaji kutoka  sehemu mbalimbali duniani kuja  kuwekeza  kwenye  Mkoa wa Singida kwa kuwa  Mkoa huo umebarikiwa kuwa na  fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo bado hazijatumika kikamilifu. 

Akifungua Kongamano la Mwongozo wa Uwekezaji kwenye Mkoa wa Singida  kabla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo huo, Dkt. Nchimbi amesema  Mkoa wa Singida  ni miongoni mwa  mikoa michache nchini  ambayo  endapo fursa  zake zikitumika utachangia  katika maendeleo ya Mkoa na nchi kwa ujumla 

Amezitaja baadhi ya fursa zilizopo kwenye  Mkoa wa Singida kuwa ni  pamoja na nishati ya mafuta asilia na gesi, madini, kilimo cha alizeti,  korosho,utalii, ufugaji wa nyuki na  kuku pia uwekezaji kwenye sekta ya michezo ambapo amesema ni zamu ya Mkoa wa Singida  kuchangia  kikamilifu kwenye uchumi wa nchi.  

Akitoa  mada kuhusu Uwekezaji wa  Alizeti mkoani Singida, Mratibu wa Utafiti wa Alizeti nchini, Frank  Reuben  amesema zao la alizeti ndiyo zao pekee linaloweza kuuvusha  mkoa  wa Singida  kwa kuwa tafiti zinaonyesha kuwa  mkoa wa Singida  ndiyo unaongoza hapa nchini kwa  kulima zao hilo. 

Ametaja  baadhi ya  maeneo ya fursa za uwekezaji kwenye kilimo cha Alizeti kuwa ni pamoja na uzalishaji na usambazaji wa mbegu, Kilimo bora (mesto) cha alizeti na ufugaji nyuki (Agro-apiculture) na uendelezaji wa viwanda vya kuchakata alizeti, chakula cha mifugo na mazao ya nyuki 

Mtafiti wa zao la Korosho, kutoka Taasisi ya Utafiti wa mazao ya Kilimo (TARI) Dkt. Fortunatus Kapinga  akitoa mada ya zao la Korosho nchini amesema  Mkoa wa Singida una ardhi nzuri yenye rutuba ambayo inafaa sana kwa zao la korosho  ukilinganisha na mikoa mingine  hapa nchini hivyo ni fursa pekee kwa  wawekezaji kuja  kufanya uwekezaji katika mkoa huu. 

Amezitaja  baadhi ya bidhaa zinazopatikana kwenye zao la Korosho kuwa ni pamoja na juisi, jamu,mvinyo, maziwa na siagi ambapo amesema kauli mbiu ya mkoa kwenye uwekezaji kwamba   “ni zamu yetu” ikitafsiriwa kwa vitendo italeta mageuzi makubwa  katika mkoa wa Singida na taifa kwa ujumla. 

Mwenyekiti wanawake wachimbaji Madini Mkoa wa Singida, Martha  Kayaga amepongeza Serikali ya awamu ya Tano inayoongizwa  na Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa  inayofanya  kuwashilikisha  wachimbaji wazawa kwenye sekta ambapo ameiomba Serikali kuangalia namna bora ambayo itawawezesha wajimbaji wadogo wadogo kupata  mitaji hususan  vifaa ili waweze  kuongeza tija katika sekta  hiyo. 

Pia Bi. Kayaga ameiomba Serikali  kuwaangalia wachimbaji wanawake kwa jicho la pekee kwa kuwa  wao  ni nguzo muhimu kwenye familia na kwamba asilimia 10 inayotengwa kwenye Halmashauri imekuwa ikielekezwa kwenye sekta nyingine ambapo amesisitiza endapo itaelekezwa kwa akina mama wachimbaji wadogowadogo itasaidia kuinua hali za uchumi kuanzia kwenye ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wake, Afisa  Uhamasishaji Uwekezaji  Mkuu kutoka  Kituo cha Uwekezaji nchini, JoyceShundu  akiwasilisha  mada ya “Mazingira na Fursa za Uwekezaji Nchini”  amepongeza  jitihada na mikakati mbalimbali inayofanywa na Mkoa wa Singida kwa kwenye uwekezaji  na kutoa wito kwa wawekezaji kuwahi kuwekeza kwenye  fursa za kipekee zinazopatikana mkoani hapa. 

Awali katika salamu za utambulisho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Lutambi amewataka Watendaji wote wa Serikali Mkoa wa Singida kuhakikisha wanajituma kufanya kazi kwa weledi kwenye utoaji huduma  bora kwa wawekezaji ili azma ya Serikali ya kutaka uwekezaji wenye tija itimie na maisha  bora kwa watanzania ifikiwe. 

Dkt. Lutambi amesema Serikali ya Mkoa imeshaandaa mazingira wezeshi kwa  wadau na wawekezaji makini kuja kuwekeza  kwa kuzingatia sheria  na taratibu za nchi.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: