Naibu Waziri wa Wizara ya Muungano na Mazingira Mwita Mwikabe Waitara leo amefanya ziara katika Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro na kutembelea Miradi ya Ujenzi wa Dampo jipya linalojengwa katika Eneo la Mtakuja mjini hapo na Pia Ametembelea mradi wa uzalishaji wa Mbolea ya Mboji itokanayo ya takataka za mabaki ya mazao na mbogamboga.


Katika ziara hiyo Mheshimiwa Waitara ameipongeza manispaa hiyo kwa kuendelea kuongoza kitaifa katika suala la usafi wa mazingira kwa miaka mfululizo sasa.


Naibu waziri waitara pia amewataka Viongozi wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Mstahiki Meya Juma Raibu kuwachukulia sheria kali na kuwashugulikia watumishi wazembe wanaopelekea kurudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano,Waitara ameendelea kusema anamfahamu Juma Raibu kabla hajawa Meya kipindi akiwa miongoni mwa Madiwani watatu wa CCM kipindi manispaa hiyo ikiwa chini ya usimamizi wa Chadema na alikuwa akisimamia misimamo ya kizalendo kwa lengo la kufanikisha manispaa hiyo kupiga hatua bila kuogopa jambo lolote.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: