Atoa siku 30 kwa mgodi wa dhahabu Geita kulipa fidia wananchi walioathirika na shughuli za uchimbaji za mgodi huo


Na. Steven Nyamiti, Geita


Waziri wa Madini, Doto Biteko  ametaja majina matatu ya wafanyabiashara  wakubwa wa dhahabu (Dealers) wanaoshiriki  katika vitendo vya  utoroshaji Dhahabu ndani ya Mkoa wa Geita.


Ametaja majina hayo kuwa ni mfanyabiashara wa Dhahabu Maduka Mbaraka, Makandaga Sita na Makaranga Kiserya.


Ametaja majina  hayo leo Desemba 29, 2020 alipofanya ziara na kutembelea Soko la Madini la  Mkoa wa Geita, pamoja na kukutana na kuzungumza na Wafanyabiashara Wadogo (Brokers) na Wafanyabiashara wakubwa wa Madini (Dealers) katika ukumbi wa Mwalimu nyerere katika Kituo cha uwekezaji cha mjini Geita (EPZA) na kuwataka kutojihusisha na utoroshaji wa madini nchini.


Amewaeleza  kuwa, tayari amepata majina 

ya wafanyabiashara wa madini sita katika mkoa wa huo wanaosifika kwa utoroshaji wa Madini lakini  ameamua kutaja majina matatu kwanza na mengine matatu  ameyahifadhi .


Amesema wafanya biashara hao wananunua Dhahabu nje ya masoko na kuuza kusikojulikana kinyume na sheria zinazosimamia sekta ya madini nchini.


Ametoa onyo la mwisho kwa wafanyabiashara hao na kuwataka  wajirekebishe vinginevyo  hatua kali zinatachukuliwa dhidi yao ikiwemo kuwafilisi Mali zao pamoja na kuwafikisha mahakamani.


"Ninawaomba tuheshimu taratibu zilizowekwa na Serikali katika kusimamia Sekta ya Madini, ifike kipindi tuone fahali kulipa Kodi. 


Amebainisha kuwa,  kwenye Maonyesho ya Madini 

Yanayotegegemewa kuyafanyika Mwaka 2021 tunzo  kwa Wafanyabiashara  wanaofuata utaratibu mzuri wa kulipa Kodi zitatolewa na kuwataka kujiandaa kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.


Amesema kuwa Rais Dkt.John Magufuli aliwafutia Kodi na tozo nyingi  za madini ambazo zilizofikia takribani asilimia 21 ili waweze kufanya biashara hiyo pasipo  kutorosha madini.


Aidha, Biteko ametaja kiwango Cha Kodi wanacholipa kwa mujibu wa sheria kuwa ni asilimia Saba pekee, kiwango ambacho ni rafiki kwa kila mfanyabiashara wa madini.


"Tukikukamata unatorosha Madini, tunachukua leseni, nadhani mmeona yaliyotokea Chunya tumefuta leseni.

Share To:

Post A Comment: