Saturday, 5 December 2020

WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU WATEMBELEA MRADI WA SGR

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akizungumza na wahasibu na wakaguzi wa hesabu kuhusu namna walivyojipanga kwenye Ujenzi wa Reli ya Kisasa maaarufu kama Standard Gauge Railway (SGR) katika eneo la Kamata jijini Dar es Salaam wakati wa kuanza kwa ziara ya utembeleaji wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme iliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akitolea ufafanuzi kuhusu Kituo cha abiria cha Reli ya Kisasa maaarufu kama Standard Gauge Railway (SGR) cha Soga kitakavyofanya kazi wakati wa ziara ya utembeleaji wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme iliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) .
Muonekano wa Kituo cha abiria cha Reli ya Kisasa maaarufu kama Standard Gauge Railway (SGR) cha Soga 
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakiwa kwenye Ziara wakati wa utembeleaji wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme iliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) .
Safari ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu ikiendelea 
 Mhandisi wa mahandaki  wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR) Kilosa, Amir Said akizungumza na wahasibu na wakaguzi wa hesabu kuhusu Ujenzi wa Mahandaki ya Reli yatakayopitisha Treni ya Kisasa ya Umeme Standard Gauge katika eneo la Kilosa mkoani Morogoro wakati wa ziara ya utembeleaji wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Umeme iliyoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) .
Meneja Mradi msaidizi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa(SGR) Morogoro- Makutupora, Mhandisi Christopher Mangwela akiwatolea ufafanuzi wahasibu na wakaguzi wa hesabu kuhusu namna walivyoweza kujenga handaki ya Reli yatakayopitisha Treni ya Kisasa ya Umeme Standard Gauge lenye urefu wa kilometa 1.1 katika katika eneo la ujenzi wa mradi wa miundombinu ya Treni ya Kisasa ya umeme SGR pembezoni mwa mto Mkondoa Kilosa mkoani Morogoro.
Baadhi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu wakitembela handaki la Reli litakalopitisha Treni ya Kisasa ya Umeme Standard Gauge lenye urefu wa kilometa 1.1 katika katika eneo la ujenzi wa mradi wa miundombinu ya Treni ya Kisasa ya umeme SGR pembezoni mwa mto Mkondoa Kilosa mkoani Morogoro.
Wahasibu na wakaguzi wa hesabu wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea Handaki ya Reli litakalopitisha Treni ya Kisasa ya Umeme Standard Gauge lenye urefu wa kilometa 1.1 katika katika eneo la ujenzi wa mradi wa miundombinu ya Treni ya Kisasa ya umeme SGR pembezoni mwa mto Mkondoa Kilosa mkoani Morogoro. Ziara hii imeratibiwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Ujenzi ukiendelea

No comments:

Post a Comment