Na Woinde Shizza,Arusha.


Askari polisi  watatu na raia sita akiwepo mfanyabiashara wa  madini Lucas Mdeme, wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha, kwa tuhuma za kumteka na  kumuomba rushwa n  Mwenyekiti wa chama cha wauzaji wa madini Tanzania(TAMIDA) Sammy Mollel .


Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Salum Hamduni,alisema tukio hilo limetokea Desemba 14,mwaka huu na kuwataja waliokamatwa ni  Askari namba H.125 Gasper Paul  kitengo cha Intelijensia Makao makuu ya Polisi Dodoma.


Wengine ni  Askari namba G 5134 DC Heavenlight Mushi  wa kitengo cha Intelijensa Mkoa wa Kinondoni na Askari namba  H.1021PC Bryton Murumbe kutoka Dodoma.


Kamanda Hamduni aliwataja wengine waliokamatwa ni pamoja na  Mfanyabiashara wa madini,Lucas Michael Mdeme(46) ambaye ni meneja kampuni ya  kuuza madini ya  CROWN Lapidary Ltd yajijini Arusha,Shabani Benson(49) mfanyabiashara wa dodoma na Nelson Lyimo(58) mfanyabiashara wa  Kimandolu Arusha.


Watuhumiwa wengine ni  Leonia Joseph(40) Sekretari wa kampuni ya Germs & Rocks Ventures,Omary Mario(43)mfanyaviashara wa eneo la Olorieni Arusha na Joseph Chacha(43) mfanyabiashara wa Elboru Arusha.


Alisema awali polisi iliwakamata watuhumiwa watatu, wakiwepo polisi wawili DC Muchi,PC Murumbe na mfanyabiashara Benson  ofisi ya Germs & Rocks baada ya kuenda kushawishi na kupokea rushwa na baadaye kukamatwa watuhumiwa wengine sita


Alisema taarifa za awali zinadai kuwa watuhumiwa hao, waliomba rushwa ya sh 30 milioni na walipokea tayari fedha sh 10milioni na kisia kilichobaki walipofuata ndio walikamatwa.                     


 Mollel alikiri kukamatwa na watuhumiwa hao, ambao walikuwa na silaha na kuondoka nae kuelekea Dodoma na wakiwa njiani kabla ya kufika Dodoma ndipo waliomba fedha .


Hata hivyo, alisema kwa sasa hawezi kufafanua zaidi tukio hilo, kwani bado uchunguzi unaendelea na watuhumiwa bado wanakamatwa.


"Huu ni mtandao mkubwa wametapeli wafanyabiashara kadhaa hivyo vyombo vya usalama vinafayakazi"alisema


Mmoja wa watuhumiwa hao,Mdeme ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa TAMIDA na meneja wa kampuni anayofanyakazi ya Crown Lapidary  ltd iliwahi kutajwa katika kesi ya Utoroshaji madini katika uwanja wa kimatataifa wa kilimanjaro.


 Mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia,Raia wa India, Anarag Jain(44) akitorosha madini gramu 2015.59  yenye thamani ya dola 310,137.255 (Sawa na Sh 670 milioni).


Baada ya kukamatwa  na madini kutaifishwa mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga  iliitaja kampuni ya  Crown Lapidey inayomilikiwa na Raia wa Kenya,Rajan Verma kuwa  ndio ambao walihusika kumuuzia mfanyabiashara huyo madini na kuahidi kumsadia kutorosha.


Mdeme alitajwa mahakamani kuhusika  kuwarubuni maafisa wa usalama wa uwanja huo na wafanyakazi, Askari E.3985D/CPL Endrew ,Caphace Rangia ,Rachel Shao, na Debora Komba kumuingiza ndani ya uwanja huo lakini baadaye madini yalikamatwa.


Watuhumiwa ha wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: