Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetolewa na serikali kukamilisha mradi wa maji Matwiga Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ili vijiji nane vianze kunufaika na mradi katika awamu ya kwanza.




Mahundi ameyasema hayo Kijiji cha Matwiga katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Mbeya.


Naye Mbunge wa Lupa Masache Kasaka mbali ya kuipongeza serikali amesema wananchi waulinde mradi huo.


Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha


Aidha Mkurugenzi wa Wakala wa Maji nchini Clement Kivegalo amesema mabomba yote yametengenezwa nchini na yamefika eneo la mradi huo.


Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka Simon Mayeka amesema wanaoharibu vyanzo vya maji watachukuliwa hatua…


Mradi wa maji Matwiga utakapokamilika utasambaza maji katika vijiji kumi na sita hivyo kuwaondolea adha wananchi wa vijiji hivyo ambao hawana maji ya bomba tangu kupata uhuru.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: