Friday, 27 November 2020

TULIA ACKSON AKAGUA UJENZI WA KIVUKO CHA RELI

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa kivuko cha relini kinachounganisha barabara ya kata za Tembela, Mwasanga na Mwakibete ambacho kimekuwa kero kwa muda mrefu kwa Wananchi wa kata hizo kukosa mawasiliano ya barabara hususani vipindi vya mvua baada ya daraja kuu lililokuwa likitumika kuvunjika miezi kadhaa iliyopita.


Akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na TARURA, Dr. Tulia amesema>>> ”Kipindi hiki ni cha mvua na sisi tuliahidi katika kampeni zetu kwamba ni lazima tupate njia mbadala ya kupata mawasiliano kwasababu daraja letu lile tangia limevunjika halijatengamaa hadi leo na wote ni mashahidi lilisababisha na vifo vya watu, kwahiyo tunaendelea kufuatilia ili kupata mbadala kwasababu mvua zinakaribia tena kuanza”


“Sisi tulianza kwa kutengeneza daraja la muda lakini sio salama sana na ndio maana tumeamua kuja kufuatilia maendeleo ya kivuko hiki mapema kabisa ili tuweze kushughulika nalo na tayari wenzetu TAZARA pamoja na TARURA wameshakubali kutusaidia kuweka mambo sawa ili kivuko na barabara hii iweze kutumika” -Dr. Tulia Ackson


“Kuhusu lile daraja la awali lililovunjika tayari umeshafanyiwa upembuzi yakinifu na tayari imefikia sehemu nzuri hivyo tusiwe na wasiwasi lile daraja litatengenezwa kwa uzuri zaidi ili kuweza kusaidia mawasiliano baina ya kata hizi tatu za Tembela, Mwasanga pamoja na Mwakibete”-Dr. Tulia Ackson

No comments:

Post a comment